WANAVYUO WASHAURIWA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI | Tarimo Blog

 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Uthibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) Bw.Henry Bantu akifungua Jukwaa la wakati wa Uzinduzi wa jukwaa la Uniforum uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mhasisi wa Jukwaa la wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Unforum) Bw.Faizak Musa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la wakati wa Uzinduzi wa jukwaa la Uniforum uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Baraza la Ushauri Watumiaji wa Huduma za Usafiuri Ardhini (LATRA CCC) wakifuatilia Uzinduzi wa jukwaa la Uniforum uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


WANAVYUO nchini wameshauliwa kutumia vyema elimu yao katika kutatua changamoto inayoikabili jamii ikiwemo kuongeza ubunifu katika Sekta Usafirishaji ili kuhakikisha jamii inanufaika na elimu yao.

Ushauri huo umetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Uthibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) Bw.Henry Bantu wakati wa Uzinduzi wa jukwaa la Uniforum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema wanafunzi ni miongoni mwa wadau muhimu wa kutoa elimu juu ya sekta ya usafiri na usalama barabarani hivyo kupitia wanavyuo elimu itawafikia wananchi kwa ukubwa zaidi.

“Kupitia wanafunzi kunaweza kusaidia kupaza sauti kwa wengine wakafahamu umuhimu wa kuzingatia sheria za barabarani ili kuweza kupunguza ajari za mara kwa mara”. Amesema Bw.Bantu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri Watumiaji Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) Dkt.George Makuke amesema wanampango wa kufikia vyuo vyote vilivyopo nchini ambapo mpaka sasa wameshwafikia wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari na sasa wameanza na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadae kufikia vyuo vingine.

“Tumeanza UDSM nadhani tutafanya vyuo vingine kama sio vitatu au vinne katika mwaka huu 2021 lengo  letu kuhakikisha wanafahamu suala la usalama barabarani na wao kuwa mabalozi wazuri kwa wengine”. Amesema Dkt.Makuke.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri Watumiaji Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC ) Bw.Leo Ngowi, amesema kuwa lengo la uzinduzi jukwaa hilo kuhakikisha wanawapa fursa wanafuzi pale wanapopata changamoto au maoni ili waweze kufikisha katika baraza kupitia wanavyuo.

Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti Mhasisi wa Jukwaa la wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Unforum) Bw.Faizak Musa amesema wao kama wanafunzi ni wadau wakubwa wa vyombo vya usafiri kwahiyo kuwepo kwa jukwaa hilo kutawapa fursa za kutoa maoni na ushauri kwa Serikali kuhusu utoaji huduma za usafiri.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2