HAJI MANARA ATEMWA SIMBA SC | Tarimo Blog


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KLABU ya Soka ya Simba rasmi imetoa taarifa ya kuachana na Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Klabu hapo, Haji Sunday Manara leo hii, ikielezwa kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu imeridhia ombi la Manara la kutoendelea kuhudumu katika nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa mapema leo, imeeleza kuwa nafasi hiyo atakaimu Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Ezekiel Kamwaga kwa kipindi cha miezi miwili, pia imeeleza kuwa atashiriki katika maboresho ya Muundo wa Utendaji wa Idara hiyo kwa kipindi chote atakachokuwepo Klabuni hapo.

Bodi hiyo imemshukuru Manara kwa kutoa taarifa ya kuwaaga Wanasimba kupitia Kundi la Viongozi wa Smba HQ, pia Klabu imemshukuru Manara kwa kipindi chote alichokuwa Klabuni hapo, hata hivyo Simba SC imesema baada ya maboresho ya Kitengo hicho itatangaza fursa za ajira katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Hatua ya kuondolewa Haji Manara katika nafasi hiyo imekuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwepo kwa sintofahamu Klabuni hapo baina yake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2