Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa, sekta ya mifugo nchini inachangia uchumi wa nchi kwa zaidi ya asilimia 7.4 na kwamba mwaka huu wa fedha unaoisha, sekta hii imekuwa kwa asilimia 5 lengo likiwa kufikia mara mbili zaidi kwenye mchango wa uchumi na kuweza kufikia angalau asilimia 15 ifikapo mwaka 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Juni 30,2021 wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Akifafanua namna sekta hiyo inavyokuwa Prof. Gabriel amesema uzalishaji wa maziwa nchini umefikia bilioni 3.4 ikiwa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni 75 hali unayoonyesha kuwa wawekezaji wengi huja kuchakata na kuleta thamani kwani wateja wananunua maziwa ambayo yameongezwa thamani .
Amesema takwimu zinaonesha katika lita bilioni 3.4 za maziwa, lita bilioni 2.38 yanatokana na Ng'ombe wa kienyeji hivyo, na hivyo ni lita bilioni 1.2 tu ndio ¹ zinatokana na ng'ombe wa maziwa". Amesema Prof. Ole Gabriel.
Aidha amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ambapo inazaidi ya ng'ombe milioni 33.9 na mbuzi wameshafika zaidi ya milioni 22 wakati kondoo wamefika takribani milioni 6, huku kuku wakiwa milioni 87.7.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Neema Mrema amesema kuwa kupitia mradi huo wana matokeo mazuri wameyaona ambapo kuna ng'ombe 558 tayari wana mimba na wengine tayari wameshapata watoto pia kuna ng'ombe 336 ambao wameogeshwa kitaalamu na vilevile kuna ng'ombe 62 ambao hao wamepata chanjo kuanzia mbili na kuendelea.
"Wauza pembejeo hawa wameweza kuwafikia wafugaji 2776 na kuuza pembejeo nne ambazo ni vidhibiti vimelea, Chanjo, lishe uhimilishaji pia mpaka sasa tuna ng'ombe 17,000 ambao wamepata huduma mbalimbali za lishe katika kuongeza afya bora na pia kuweza kupata maziwa yaliyobora". Amesema Neema
Amesema kuwa mradi huo una malengo matatu ambapo lengo la kwanza ni kuongeza uzalishaji na tija ya maziwa kwa wafugaji wadogowadogo, kuongeza kipato kwa wafugaji wadogowadogo wa maziwa, kuleta uwiano sahihi na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa shughuli katika sekta ya maziwa .
"Washiriki sita wa mradi huu kutoka sekta binafsi wamepata tuzo na motisha za dola za kimarekani 27,000 kwa pembejeo 4116 zilizokamilika ili waweze kuendelea kutoa huduma na kuongeza uzalishaji wa maziwa na kukidhi soko la Tanzania." Amesema.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel, akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta ya mifugo wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji sita wa pembejeo waliochaguliwa kushiriki kutoa huduma za Ugani kwa Wafugaji wa maeneo ya Pwani, Dar es Salaam, Morogoro na Tanga.
Mratibu wa Mradi wa AgResults Tanzania Dairly Productivity Challenge Neema Mrema akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo sita waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaa, Pwani, Morogoro na Tanga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Steve Michael akizungumza wakati wa hafla ya kuwapatia vyeti wauza wa pembejeo jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo nchini wakifuatilia hafla ya kuwapatia vyeti wauzaji sita wa pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji maeneo ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga.
Baadhi ya wauza wa pembejeo waliochaguliwa kushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa wafugaji walioko maeneo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga wakikabidhiwa vyeti mara baada ya kufanya vizuri katika sekta hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment