Taasisi elimu ya juu zalisheni watalam wenye ujuzi: Kipanga | Tarimo Blog

Na Karama Kenyunko Michuzi TV .


SERIKALI imezitaka taasisi za elimu ya juu kutambua
kwamba bado zinakazi kubwa ya kuongeza wataalam wa kiwango cha ujuzi wa juu na kati kwani bado taifa halina wataalam wa kutosha katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo wenye kiwango hicho cha elimu hususani katika masuala ya sayansi na teknolojia.

Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga, ameyasema hayo leo Julai 31, 2021wakati wa kufunga maonesho ya 16 ya elimu ya juu,sayansi na teknolojia yaliyoandaliwa na TCU yenye kauli mbiu isemayo kuendelea kukuza na kudumisha uchumi wa Kati kupitia elimu ya juu sayansi na teknolojia.

Amesema ukuaji wa uchumi na mafanikio katika sekta ya uzalishaji unategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa rasilimali watu wenye ujuzi na maarifa ya kubuni na kuendeleza Teknoloji mbali mbali na kutatua changamoto zinazokabili jamii yetu na taifa kwa ujumla.

Amesema, kwa takwimu za 2016 zinaonyesha watu wenye ujuzi wa juu  ni asilimia 3.3 huku wenye ujuzi wa kati ni asilimia 17, kitu kinachoonyesha kwamba taasisi zetu za elimu ya juu bado zinakazi kubwa ya kuongeza wataalamu wa kiwango cha ujuzi wa  juu na wa kati.

"Ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi hauwezi kuwa na mafanikio yaliyokusudiwa pasipokuwepo na mchango wa elimu ya juu sayansi na Teknolojia, ili kudumu na kufikia uchumi wa kati wa juu nchi lazima iwe na watu wenye ujuzi  wa juu kwa asilimia 12 na ujuzi wa kati kwa asilimia 26.

Naibu waziri Omary pia amezitaka taasisi za elimu ya juu za serikali na binafsi kuweka mipango itakayoongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu wenye ujuzi na ushindani katika soko la ajira na kuongeza kuwa serikali inaendekea kuboresha Vyuo mbalimbali nchin ili viweze kutoa elimu bora ya kiushindani ndani na nje ya nchi.

Aidha amezihimiza taasisi za elimu ya juu kuwekeza zaidi katika tafiti na ubunifu ambapo katika kipindi Cha miaka mitani ijayo serikali imedhamiria kuwekeza katika sekta ya ubunifu na utafiti ili nchi iweze kupata bunifu na tafiti zenye kutatua changamoto za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha ametoa wito kwa TCU kuongeza jitihada katika udhibiti wa ubora na kufanya maboresho stahiki ili  kuhakikisha kuwa vyuo vikuu vinatoa wahitimu bora na wenye uwezo wa kuhimili ushindani katika soko la ajira.

Amesema kuwa serikali itaendelea kuenzi ubia na ushirikiano baina na sekta ya umma na sekta binafsi katika utoaji wa elimu ya juu  japa nchini kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji bila kuathiri ubora wa elimu   

Naye Katibu Mtendaji tukoka Tume ya Vyuo Vikuu Prof Charles Kihampa amesema kupitia maonesho hayo wananchi wameweza kujifunza na kuona yanayofanywa na vyuo vya elimu ya juu ikiwemo namna ya kujiunga na vyuo ambapo katika maonesho jumla ya wahitimu zaidi ya elfu hamsini na nne wameweza kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya juu ikiwa dirisha la udahili lilishafunguliwa.

Nao washiriki wa maonesho hayo ikiwemo wakala wa Vyuo Vikuu nje ya nchini-GLOBAL EDUCATION LINK wamesema kuwa maonesho hayo yamewapa nafasi kama wadau wa elimu ya juu sayansi na teknolojia kubadilishana uzoefu na kuweza kujifunza kutoka miongoni mwao na kupata mawazo mapya.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza wakati akifunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na TCU na kufanyika kwa siku sita katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (katikati) akipokelewa na wenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa TCU na Makamu Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Hurbert Kairuki Prof. Charles Mgone (wa kwanza kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa (kulia) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam kufunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na (TCU) kwa siku sita.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga (kushoto) akizungumza na Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa TCU Hilda Kawiche (kulia) alipofika kwenye Banda la Tume hiyo kupata maelezo ya namna wanavyofanya kazi zao. (wa ipi kushoto) ni Prof. Charles Kihampa Katibu Mtendaji wa TCU
Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa (kushoto) akimkabidhi Zawadi ya Vitabu Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza alipomaliza ziara fupi ya kutembelea Banda la TCU. 
Wadau Mbalimbali na Wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu wakifuatilia kwa karibu hotuba kutoka meza Kuu.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2