Takukuru Manyara yatahadharisha wananchi wanaonunua ardhi Babati. | Tarimo Blog


Na John Walter-Babati

Kutokana na baadhi ya wananchi wasio waaminifu kuuza maeneo yaliyokatazwa na serikali kutumika,Taasisi ya kuzuia na kupambna na rushwa mkoa wa Manyara imewataka wananchi kuwa makini na watu hao ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mtaa wa Miomboni mjini Babati.

Makungu amesema mwananchi anaetaka kununua ardhi katika mji huo ni bora akafuata taratibu za kisheria ili kuepuka kuuziwa maeneo ambayo hayaruhusiwi kuuzwa.

“Ni wito wetu kwa wananchi wenye utashi wa kununua maeneo kwenye mitaa ya kata za Babati,Maisaka au Nangara,kabla ya kufanya hivyo wawasiliane na ofisi ya ardhi halmashauri ya mji wa Babati au ofisi za wakala wa Barabara nchini Tanroads ili kupata uhakika wa kutouziwa eneo inakopita bara bara ya mchepuko na kuingia hasara amabayo ingeweza kuepukika” alisema Makungu

Makungu amesema Katika mji wa Babati,Serikali imepanga kujenga barabara ya mchepuko kupitia baadhi ya maeneo ya kata za Babati,Maisaka na Nangara ambapo maeneo hayo yamekwisha ainishwa hivyo yapo maeneo yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya kupitisha barabara za mchepuko kwa lengo la kuondoa msongamano wa magari katikati ya mji na kupelekea ahueni kwa watumiaji wa barabara.

Amesema Wakala wa Bara bara mkoa wa Manyara (TANROADS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji wa Babati wameshafanya mikutano kuwaelimisha wananchi wa maeneo hayo,mtaa kwa mtaa kuhusu umuhimu wa barabara hiyo, mara baada ya kuzitambua mali ambazo zinastahili kulipwa fidia katika maeneo ambamo barabara itapita huku wakielekeza wananchi wasifanye maendeleo mapya kwenye maeneo hayo.





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2