UCHAFU WATISHIA KIPINDUPINDU MONDULI | Tarimo Blog


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akiwa ameambatana na wenyeviti wa mashina na matawi wakikagua dampo lililopo ndani ya makazi ya watu katika Kitongoji cha Sinon Kusini wilayani Monduli.

Na Imma Msumba, Monduli
WANANCHI wa Kitongoji cha Sinoni Kusini katika kata ya Engutoto wilayani Monduli wamemlalamikia Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen kitendo cha uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuweka Dampo la taka katika maeneo ya makazi ya watu na kutishia kutokea kwa ugojwa wa kipindupindu katika msimu wa mvua.

Bi. Lucy Laizer mkazi wa kitongoji cha Sinoni Kusini alisema kumewepo na usumbufu mkubwa na badhii ya wakazi wa Kitongoji hicho wenye watoto wadogo huwalazimu kuhama nyumba kutokana kukidhiri kwa taka katika mtaa na harufu mbaya pamoja na moshi mkali pindi wachomapo taka hizo huwaathiri kiafya na kusababisha vikohozi kwa watu wa mtaa huo.

Bi. Laizer alisema baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho cha Sinoni Kusini wamekuwa wakiadhiriwa na harufu kali na kutishia wakazi wa kitongoji hicho kupata ugonjwa wa kikohozi wakati halmashauri ikiendelea kuchoma taka katika eneo la korongo ambalo liko katikati ya makazi ya watu .

Aidha Bi laizer alienda mbali na kuulalamikia uongozi wa halmasahauri kitengo cha usafi na mazingira kwa kusema kuwa wameshidwa kutekeleza na kuendana na kauli ya Serikali ya Awamu ya sita ya kuwataka wanachi kufanya usafi ili kuweza kujikinga na magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya Engutoto Nelson Ngoyai Lowassa alikiri kuwepo na tatizo hilo katika eneo la kitongoji hicho kuadhiriwa na kadhia hiyo ambapo alisema kuwa takataka nyingi zinatupwa kwenye korongo zinazalishwa na wafanyabiashara wa sokoni na wakazi wa Mji wa Monduli na kuzitupa katika korongo hilo.

Diwani Lowassa alisema suala hilo amelifikisha katika Baraza la madiwani la Halmashauri na tayari eneo limeshapatikana hivyo ndani ya kipindi kifupi dampo hilo litahamishiwa sehemu husika maana tayari Halmashauri imeshapata eneo kwa ajili ya kuweka dampo kubwa na la kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Frank James Mwaisumbe akizungumza nasi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo nakusema "Hilo tatizo la jalala nimelikuta,ila mkumbuke ndo kwanza mgeni nina wiki mbili tu sasa hapa lakini kama mnavyojua eneo kubwa la wilaya ya monduli ni la Jeshi maeneo ya ardhi huku ni hafifu lakini tunashukuru ndugu zetu wa Jeshi la Wananchi JWTZ wameshatupatia eneo na tayari tumeanza mchakato wa kutengeza dampo kubwa na la kisasa katika eneo tulilopewa na Jeshi hivyo ndani ya muda mfupi ile adha pale kwa wananchi itaondoka" Alisema Mwaisumbe.

Muonekano wa Dampo hilo lililopo katikakati ya makazi ya wananchi wa Kitongoji cha Sinoni Kusini.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2