UKWELI KUHUSU MAPATO YA MANISPAA YA LINDI | Tarimo Blog

Manispaa ya Lindi iliongezewa eneo la Utawala kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi (Lindi DC) ambalo liliangukia kwenye Jimbo la Mchinga na Kamati ya Fedha na Utawala kwenye kikao Maalumu cha Tarehe 05/06/2020 walijadili  na kupokea mali,bajeti na watumishi wa iliyokuwa sehemu ya Lindi DC (Jimbo la Mchinga) 

Kikao hicho kwa kauli moja walikubaliana  kuhamishiwa sehemu ya bajeti ya 2020/21 ya eneo la Mchinga kwenye Manispaa ya Lindi na kufanya ukomo wa bajeti ya Manispaa hiyo kuongezeka kwa Shilingi Bilioni 1,059,227,980 na kiasi hicho hicho kupungua kwenye ukomo wa bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ambapo kwa sasa inajulikana kama Halmashauri ya Wilaya ya Mtama. 

Baada ya ongezeko hilo kwenye ukomo wa Bajeti ya Manispaa ya Lindi ilifikia kiasi cha Shilingi Bilioni 3,500,834,000 badala ya ile ya awali ya Shilingi Bilioni 2,443,320,000.

Hivyo, Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu ilijielekeza kwenye mabadiliko yaliyofanyika ya kuhamishiwa kwa eneo hilo la utawala na mali zake, ambapo hadi kufikia Juni 30, 2021, Manispaa ya Lindi imekusanya kwa asilimia 58% ya ukomo wa bajeti ya Shilingi Bilioni 3,500,834,000.

Hata hivyo, Baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamejielekeza kwenye Bajeti ya awali kabla ya kuongezewa eneo la utawala ambayo ni Shilingi Bilioni 2,443,330,000 bila kuzingatia mabadiliko yaliyofanywa.

 Kufuatia hali hii, Mhe.Waziri Ummy anawahimiza madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kuongeza jitihada za ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Manispaa hiyo ili kuweza kutoa huduma bora za jamii kwa wakazi wa manispaa hiyo ikiwemo kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2