DKT SENGATI ALITAKA BARAZA LA ARDHI WILAYA KUTANGULIZA HAKI KATIKA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO | Tarimo Blog

 Na Anthony Ishengoma –Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wajumbe wa Baraza la Ardhi wa Wilaya Mkoani Shinyanga kutambua kuwa migogoro ya Ardhi ni mibaya kuliko migogoro mingine yote hapa Nchini kutokana na uhusiano uliopo kati ya ardhi na maisha ya Binadamu.

‘’Vijana hawataki kufanya kazi wanataka kupora ardhi ya wazazi wao bado wakiwa hai  ili wachukue ardhi, matajiri wanapola ardhi ya masikini kwa njia ya rushwa ni imani yangu kwamba migogoro ya ardhi ndiyo migogoro mibaya sana kuliko mgogoro wowote hapa nchini’’. Aliongeza Dkt. Sengati.

Dkt. Sengati alisema hayo mara baada ya kuapisha wajumbe watatu wa Baraza la Ardhi la Wilaya na kuwataka wajumbe hao kusimamia haki wakati wa kufanyia kazi migogoro ya Ardhi ili wasije jitokeza tena baadhi ya watu kumfuata ofisini kwa ajili kufanya kazi hiyo wakati wajumbe wapo kwa ajili ya kazi hiyo.

‘’Tutangulize haki ya mtu mbele kiukweli na kuachana na mambo madogo madogo ambayo kimsingi yanapita na dunia inapita nataka tutende haki ili kufika mbinguni kwahiyo tutende haki. Alinukuliwa akisema Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.   

Naye Mjumbe wa Baraza hilo Bi. Eva Minja Lopa alisema kuwa watajihitahidi kufanya kazi hiyo kama ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyowaagiza na kuongeza kuwa ingekuwa kuna sehemu au chuo cha kujifunza maadili na kama kingekuwepo wange kwenda kujifunza lakini ni maadili ya mtu yanayomwezesha kufanya kazi kama hiyo.

Aidha Bw. Bernard Maduhu Itendele aliongeza kuwa atatumia weledi wake katika kazi hiyo kutoa ushauri wake kwa Mwenyekiti wa Baraza hilo ili kufanikisha yale yote yanahusu haki katika kutatua migogoro ya ardhi na kuleta ufanisi unaotakiwa katika kazi hiyo.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Bw. Paulos Lekamoi alisema kuwa uteuzi wa Baraza hilo kimsingi unafanywa na Waziri wa Wizara yake kwa kushauriana na Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa Baraza hilo uteuliwa kila baada ya kipindi cha miaka mitatu.  

Bw. Lekamoi aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa kimsingi ametoa wito ambao yeye na kamati hiyo wameuchukulia kama semina ndogo kwao na watafanya kazio kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuongeza kuwa wajumbe hao sasa watafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu kama ilivyotaratibu za Baraza hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati  akipitia moja ya kiapo cha wajumbe Baraza la Ardhi Wilaya baada ya kuwa ameapa mbele yake kwa kutumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akimwapisha Mzee Bernard Itendele kuwa mjumbe wa Baraza la Ardhi Wilaya atakayetumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akimwapisha Bi.Esha Hassan Stima kuwa mjumbe wa Baraza la Ardhi Wilaya ofisini kwake jana baada ya kuapa kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2