MKIMBIZA MWENGE ATAKA USHIRIKISHWAJI WANANCHI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO ILALA | Tarimo Blog


Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Mkimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru Maalum, Luteni Josephine Mwambashi amebaini kutoshirikishwa kwa wananchi katika miradi ya Maendeleo inayojengwa katika Manispaa ya ilala.

Luteni Mwambashi ambaye alipata wasaa wa kukaguairadi tisa ya Maendeleo ambapo alianza na mradi wa ujenzi wa kituo Cha Polisi Mzinga kilichopo katika katabya Mzinga jiji la Ilala.

Mara baada kukagua kituo hicho mkimbiza Mwenge alibaini ushikishwaji hafifu wa wananchi katika hatua Maendeleo ya ujenzi huo.

Luteni Mwambashi na Timu yake iliwachukua muda Sana kupata mukhtasari wa ujenzi wa kituo hicho jambo ambalo limewafanya kusisitiza ushikishwaji wa wananchi.

Luteni Mwambashi pia alioneshwa kutoridhishwa na hali ya ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa kituo Cha Daladala Cha kinyerezi hali iliyowazimu kukaa kwa muda mrefu kuhoji .

Mkimbiza Mwenge alioneshwa kutoridhishwa na ujenzi wa Madarasa shule ya Sekondari Kasulu iliyopo katika kata ya Ilala.

Luteni Mwambashi  alikagua risiti zilizotumika kumlipa mkandarasi na kubaini kutokuwepo kwa uwiano  wa matumizi ya fedha za ujenzi wa mradi huo

 Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Mwenge huo jana mbali na tanki la maji la Pugu ni pamoja na Daraja la Ulongoni pamoja na Barabara yake yenye urefu wa Kilomita 7.5 hadi ujenzi wa Stendi ya Segerea, kikundi cha vijana cha Kinyerezi Garden,pamoja na ujenzi wa Hospitali binafsi ya Al-Amal.

Miradi mingine ni pamoja na kituo cha mfumo wa mapato cha Jiji,ujenzi wa Madarasa 20 katika Shule ya Sekondari Kasulu,kiwanda kidogo cha kuzalisha vitafunwa kilichopo Vingunguti pamoja kiwanda kidogo  cha  kikundi cha watu wenye ulemavu kinachojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa (samani) za vyuma kilichopo katika eneo hilo.

Kiongozi wa mbio za  Mwenge Luteni Josephine Mwambashi aliwataka wasimamizi na watekelezaji wa miradi mbalimbali kuhakikisha wanawashirikisha wananchi kabla ya kuanza kwa miradi hiyo.

Kauli ya kiongozi imekuja kutokana na malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa baadhi ya wananchi hususani katika mradi wa ujenzi wa stendi ya Segerea waliolalamikia hatua ya watekelezaji wa mradi huo kutowashirikisha kabla ya kuanza kwake.

Alisema kitendo cha wasimamizi na wajenzi wa miradi hiyo kutowashirikisha wananchi kunawanyima haki yao ya msingi ikiwemo kufahamu gharama za ujenzi wa mradi husika, muda wake wa kuanza na hadi kuisha kwake.

Mwenge huo leo unatarajiwa kuanza kukimbizwa katika Wilaya ya Ubungo na kuitembelea jumla ya miradi  10 iliyopo katika wilaya hiyo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi akizungumza na Wakazi wa Vingunguti wakati wa uzinduzi wa mradi wa Bakery ya mikate
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakisoma nyaraka mbalimbali zinazohusu ujenzi wa kituo cha Daladala Kinyerezi.

Mmoja ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru akichimba chini katika kituo Cha barabara ya Kinyerezi kuangalia ubora wa barabara hiyo.

Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakikagua Daraja la Ulongoni lililojengwa katika jiji la Ilala

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Bwelaguza Ludigija akitoa maelezo kwa mkimbiza Mwenge wa Uhuru



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2