MOBETTO AWAFUNDA MISS PRIMA AFRO 2021 ASISITIZA NIDHAMU | Tarimo Blog

 
 Na.Khadija Seif , Michuzi tv

MKALI wa kibao cha Ex_wangu remix Hamisa Mobetto amewatia moyo washiriki wa Shindano la Miss Higherlearning ambayo kwa sasa yanatambulika kama Miss Prima Afro.

Hamisa amezungumza na Washiriki hao Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa jaji katika Shindano hilo Linalotarajiwa kufanyika mapema septemba mwaka huu.

"Katika mafanikio yoyote yale nidhamu ni kitu muhimu ili kufikia malengo,hivyo na wasihi kuimarisha nidhamu katika Mchuano huu ambao utaenda kubadilisha maisha yenu ya nyumbani na hata katika jamii maisha ya umaarufu una vingi hivyo tuwe na nidhamu na tusilewe sifa ."

Hata hivyo Mobetto amesema Mashabiki wategemee makubwa Sana katika Shindano hilo kutokana na kupata udhamini na Kampuni ya kutengeneza nywele (Prima afro) .

"Tutegemee tu Mazuri na Makubwa kutokana na Ushirikiano na Kampuni ambayo imenipa ubalozi hivyo zawadi itakua nono na warembo watapata faida kupitia bidhaa zetu mbalimbali za nywele aina ya Prima afro."

Kwa upande wake Muandaaji wa Shindano la Miss prima afro Adam Nkundya ametoa shukrani za dhati kwa Kampuni ambayo imeingia ubia na Kudhamini Shindano la Miss Higher learning 2021 Hadi 2022.

"Kuwepo kwa udhamini huu tutaweza kuendesha Shindano letu vizuri na tutaweza kumpatia Mshindi zawadi yake hivyo kwa kupitia udhamini huu tunategemea mengi zaidi."

Hata hivyo Nkundya amewaomba Mashabiki na wadau wa urembo kuwapigia kura Washiriki hao kupitia kurasa za prima afro.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2