MSAMA PROMOSHENI YAREJEA, TAMASHA KUBWA LA INJILI KUFANYIKA OKTOBA 3 UWANJA WA UHURU | Tarimo Blog

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama amefunguka kuwa baada ya ukimya mrefu wa takribani miaka sita wa kutoandaa matamasha ya burudani wanatarajia kufanya tamasha kubwa la nyimbo za injili Oktoba 3, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Msama ametoa kauli hiyo leo alipokua akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema tamasha hilo litakua la kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo amelivusha salama Taifa la Tanzania katika mambo magumu ambayo imepitia.

Msama amesema kuwa tamasha hilo litakua limebeba mambo mengi ambapo kadri siku zitakavyokua zinasonga mbele ndivyo ambavyo watakua wakieleza zaidi juu ya mambo ambayo yatafanyika siku hiyo.

"Tamasha hili litakua la kihistoria kwa sababu hatujafanya takribani miaka sita, niwaambie mashabiki wote waliomiss matamasha yetu kuwa tunarejea kwa nguvu kubwa na tutahakikisha kila ambaye atalipa kiingilio chake atapata burudani ya kutosha.

Kutakua na wasanii tofauti tofauti, wa ndani ya Nchi na wa nje ya Nchi, tutaalika waimbaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kila mmoja anafurahia tamasha letu," Amesema Msama.

Amesema utofauti mwingine wa tamasha hili ni kwamba halitofanyika Dar es Salaam pekee bali wamepanga lifanyike kwenye Mikoa mingine nane ili kutoa fursa kwa mashabiki na watanzania walioko nje ya Dar es Salaam kuhudhuria.

Kwa upande wake msanii wa injili nchini, Jessica Honole amesema wao kama wasanii wanamshukuru Mungu kwa kuwezesha kurudi kwa tamasha hilo tena kwani tamasha hilo limekua ni baraka kwenye maisha yao.

" Hakika tunamshukuru Mungu kurejea kwa matamasha haya, yamekua ni chachu kwa wasanii wengi wa injli nchini lakini zaidi yameokoa maisha ya wengi wapo waliobarikiwa na kuokoka kupitia matamasha ya Msama hivyo niwasihi watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Oktoba 3 pale Uwanja wa Uhuru," Amesema Jesca.

Nae nguli wa muziki wa injili, Upendo Nkone amethibitisha kushiriki tamasha hilo ambapo amewaomba watanzania wote bila kujali tofauti zao kujitokeza kwa wingi kumshukuru Mungu kupitia tamasha hilo.

" Ni muda mrefu hatujafanya matamasha haya ya shukrani, hivyo naamini Oktoba 3 tutakuja kitofauti na hakika burudani itakuepo ya kutosha hivyo watanzania na mashabiki zetu kwa ujumla wasikose," Amesema Nkone.

Mess Chengula nae ni mojawapo ya wasanii ambao wamethibitisha ushiriki wao na kutoa wito kwa watanzania wote kujitokeza katika Uwanja wa Uhuru kushuhudia kurejea kwa tamasha hilo pamoja na kupata burudani ya aina yake.

Mkurugenzi wa Msama Promosheni , Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),leo Agosti 21,2021 jijini Dar alipokuwa akieleza kuhusu ujio wa tamasha kubwa la kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 3 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar
Mmoja wa Waimbaji nyota wa muziki wa injili Upendo Nkone (wa tatu kulia) akiimba kwa hisia moja ya wimbo wake mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha  kubwa la Kumshukuru Mungu litakaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promosheni,Oktoba 3,2021 katika uwanja wa Uhuru,Kulia ni Mwimbaji mwingine mahiri aitwaye Mess Chengula na kushoto ni Jessica Honole
Mmoja wa Waimbaji nyota wa muziki wa injili nchini, Upendo Nkone ( kushoto ) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu namna atakavyojiandaa na atakavyolinogesha tamasha kubwa la Kumshukuru Mungu litakaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promosheni,Oktoba 3,2021 uwanja wa Uhuru,Kulia ni Muandaaji wa tamasha hilo Ndugu Alex Msama akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa ukumbini humo.

 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2