MTEJA AIKALIA KOONI KAMPUNI YA VODACOM | Tarimo Blog

KUFUATIA juhudi za kumaliza mgogoro kati ya Vodacom na mteja wake, Fransis Mosha juu ya kesi ya madai  iliyofunguliwa na Mosha akiidai kampuni hiyo fidia ya Sh. Milioni 26 kushindikana, Mahakama imewataka wadaawa hao kufika Mahakamani Septemba 16,2021 kwa ajili ya kuanisha hoja zinazobishaniwa

Pia siku hiyo wadaawa pamoja na Mahakama watapanga muda utakaofaa shauri hilo la madai namba 57 ya mwaka 20 kusikilizwa mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Aron Lyamuya amesema hayo leo Agosti 18 2021 wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Mapema, wakili wa Mosha, Michael Merere alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo iliishia kwenye hatua ya usuluhishi ambapo haikufikiwa muafaka  hivyo waliiomba mahakama kutoa hoja na kuipangia tarehe ya kuendelea.

Awali mteja wa Kampuni ya Vodacom Francis Mosha alifungua kesi ya madai dhidi ya Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania akidai fidia ya shilingi Milioni 26 kwa kumkata kiasi cha shilingi 2936 kwenye akaunti yake ya M-Pesa.

Katika madai yake, Mosha kupitia wakili wake Michael Merere anadai kwambaJanuari 8, 2020 bila sababu za msingi kupitia akaunti yake ya M-pesa kiasi cha sh. 20,000 kilikatwa na kwamba tatizo hilo lilijirudia Januari 9, 2021 ambapo kiasi cha shilingi 9136 kilikatwa kutoka katika akaunti yake ya M-Pesa.

Anadai baada ya Matukio hayo mawili mlalamikaji aliwasiliana na muhudumu wa Vodacom ambaye alimweleza tatizo hilo litafanyiwa kazi, lakini miezi mitatu ilipita na hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na Vodacom.

Kufuatia hali hiyo ya uzembe wa Vodacom au kushindwa kutilia maanani madai yake mdai, aliamua kuajiri Mwanasheria ambaye alipeleka madai kwa walalamikiwa, pamoja na kupolekewa barua hiyo, majibu ya Vodacom yalikuwa si ya kurudhisha kwa kuzingatia kuwa pesa za Mdai hazikurudishwa kwa takribani miezi minne, kitendo hicho kilimsababishia hasara hiyo.

Kufuatia hasara hiyo Mosha anaiomba Mahakama waiamuru Vodacom imlipe fedha hizo kiasi cha shilingi 26496320.

Hata hivyo katika majibu ya Vodacom Tanzania kupitia wakili wake Elizabeth Chacha wamekanusha madai hayo na kuwasilisha pingamizi la awali wakiiomba Mahakama itupilie mbali ombi hilo kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Pia anadai kuwa madai hayo si ya kweli na kwamba hakuna hasara yeyote ambayo Mdai ameipata kwa sababu hela hizo zilikatwa kimakosa na zilisharudishwa.

Kesi itaendelea Septemba 16 Aprili.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2