RC TABORA AAGIZA UFUNGAJI WA MIFUMO TEHAMA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAPATO KATIKA MAENEO YA KUTOA HUDUMA ZA AFYA | Tarimo Blog


NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza kufungwa kwa Mfumo wa wa utoaji wa taarifa katika vituo vya Serikali vya kutolea huduma za afya GOTHMIS ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Alisema kukosekana kwa Mifumo huo katika baadhi ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya za Seikali kumesababisha upotevu wa fedha za umma nakuishia mifukoni mwa watu wachache.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo mjini Tabora baada ya kukutana na Wajumbe wa Baraza la Watu wanaishi na VVU Tanzania na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Kaspar Mmuya

Alisema katika Zahanati ambazo zimeanza kutumia mfumo GOTHIMS mapato yao yamepanda mara mbili.

“Kuna Kituo cha Afya wilayani Urambo waliokuwa wakipata kiasi cha shilingi laki tatu kwa mwezi lakini baada ya kufunga mfumo wa GOTHIMS mwezi wa kwanza mapato yalipanda na kufikia milioni saba na Mwezi uliofuata walipata milioni 10…hii inaonyesha kuwa fedha nyingi zilikuwa zikiishia mifukoni mwa watumishi wasio waaminifu”alisema

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amewaonya Wahasibu kutoharibu mifumo kwa ajili ya kutaka wakusanye mapato kwa mfumo wa zamani.

Alisema ikibainika watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya Sheria.
Mkuu wa Tabora Balozi Batilda Buriani (kushoto) akiwa katika picha pamoja leo na  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Kaspar Mmuya (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo .

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2