TUTAENDELEA KURUDISHA KWA JAMII NA KUTHAMINI MCHANGO WA WAFANYABIASHARA- MSALILWA | Tarimo Blog



KATIKA Kuhakikisha jamii na wateja wanapata faida ya uwepo wa kampuni ya Cocacola Tanzania nchini kampuni hiyo imeendelea kurudisha fadhila kwa jamii na wateja wao kwa kutoa faida itokanayo na mauzo ya vinywaji kwa kutoa zawadi za pikipiki za miguu mitatu (tuku-tuk) kwa wateja wa jumla ikiwa ni sehemu ya shukrani pamoja na kushiriki katika ujenzi wa taifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi kwa wateja wa jumla wa vinywaji mkoani humo Mkurugenzi wa Mikakati na Ukuaji wa Kampuni Josephine Msalilwa amesema waliotunukiwa zawadi hizo  wateja wa jumla ambao wengi wao wametokea  Manzese na wamekuwa wafanyabishara wakubwa wenye kushirkiana na kampuni hiyo katika kuleta maendeleo kwao na jamii kwa ujumla.
 
Bi. Msalilwa amesema kuwa mchakato huo haukuwa wa ushindani bali kampuni hiyo imetambua mchango wa wateja huo na kwa namna ya pekee wakaoana ni vyema kushiriki kwa ukaribu zaidi kwa kutoa usafiri huo ambao utawasaidia katika usambazaji wa bidhaa za vinywaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mauzo Eric Ongara amesema zawadi hizo kwa wateja wa jumla zilihusisha wateja  50  na waliangalia mauzo yao ndani ya kwa miezi minne iliyopita hatimaye kujishindia zawadi hizo ambazo zitawasaidia katika usambazaji wa bidhaa zao.

Amesema zawadi hizo zenye thamani ya milioni 15, shilingi milioni 5 kwa kila pikipiki  zimetolewa ikiwa ni sehemu ya shukrani na kutambua thamani ya wateja hao.

Vilevile amesema kuwa, Cocacola Tanzania  itaendelea kuwatambua wateja wanaofanya vizuri na kurudisha kwa jamii kupitia faida zinazopatikana pamoja na kuhakikisha jamii inapata huduma bora.








Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni ya Cocacola Tanzania Eric Ongara akizungumza katika hafla hiyo na kueleza kuwa zawadi hizo ni sehemu ya shukrani na kutambua thamani ya wateja wao leo mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ukuaji wa Kampuni Josephine Msalilwa akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi hizo na kueleza kuwa wataendelea kutoa huduma bora pamoja na kurudisha kwa jamii, Leo mkoani Dar es Salaam.


Baadhi ya wakazi wa Manzese wakishuhudia utoaji wa zawadi hizo.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2