Watu 9 mbaroni kwa wizi wa vipuri kwenye kiwanda cha dawa na vifaa tiba Njombe | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Jeshi la polisi mkoani njombe linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa miundombinu ya vipuri kutoka kwenye kiwanda cha serikali cha dawa na vifaa tiba kinachoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Akitoa taarifa ya mafanikio ya kupatikana kwa vipuri aina ya mota nne kwenye wilaya ya kipolisi mjini Makambako,kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issa amesema tayari jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwemo walinzi wa kiwanda hicho kilichopo katika kijiji cha idofi mjini makambako.

“Kiwanda hiki hakijaanza kufanya kazi lakini kuna baadhi ya wtumishi na wananchi wanaokaa maeneo ya karibu na kiwanda wameweza kushirikiana na kuiba baadhi ya vipuri katika hawa watu tisa kuna walinzi wako mle,waliozinunua,waliozihafadhi na kuna waliozidalalia”alisema Kamanda Issa

Kutokana na jitihada za jeshi la polisi kufanikisha kupatikana kwa vipuri hivyo vilivyoibwa, kamanda issa ametoa wito kwa baadhi ya wananchi na wataalam mkoani njombe waliopewa dhamana ya kujenga na kusimamia miradi ya maendeleo kuwa waadilifu na wazalendo.

“Yeyote anayepangiwa kazi ya ulinzi tanguliza uzalendo na uaminifu katika kazi ya ulinzi na sio vinginevyo”aliongeza kamanda Issa

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa na vifaa tiba, mhandisi Shiwa Mushi amezungumzia namna walivyobaini wizi wa vipuri hivyo.

“Kwa hiyo kupatikana kwa Motor hizi kuna kazi zitaweza kukamilika vizuri,tunaomba wananchi na wafanyakazi tuweze kushirikiana ili kukamilisha ujenzi huu na ukikamilika utaweza kuajili watu 100 hii ni kazi ya nchi”alisema mhandisi Shiwa Mushi.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2