WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA KIWANJA KILICHOKABIDHIWA KWA TBA KWA AJILI YA KUJENGA JENGO KUBWA LA OFISI YAKE KWENYE MJI WA SERIKALI MTUMBA JIJINI DODOMA | Tarimo Blog

 

Eneo la kiwanja cha Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilichopo kwenye Mji wa Serikali ambacho jengo kubwa la ofisi hiyo litajengwa na Mkandarasi TBA kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi WHC. Katikati ya kiwanja hicho ni wataalam wa TBA na WHC wakijadiliana kuanza ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (wa kwanza kulia) akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (mwenye barakoa) mipaka ya kiwanja ambapo Ofisi ya Rais-UTUMISHI itajenga jengo kubwa la ofisi kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia kwa Mhe. Waziri) na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Musa Magufuli (wa kwanza kushoto).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa maelekezo ya ujenzi wa wa jengo kubwa la ofisi yake kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Wanaopokea maelekezo hayo ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kushoto),  Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael (kushoto kwake) na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa ofisi yake Bw. Musa Magufuli (kulia kwake).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwasili kwenye kiwanja ambacho ofisi yake imemkabidhi Mkandarasi TBA na Mshauri Mwelekezi WHC kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo kubwa la ofisi yake kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Waliombatana nae ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia kwake) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael (kushoto kwake).


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2