Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene kushoto akimpongeza Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo, afya na Elimu.
Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) kilichopo chini ya mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) akiwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene akiwa Katika picha ya pamoja na Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Picha ya pamoja.
Picha mbalimbali zikionesha Washiriki wa kongamano Hilo waliokuwemo Katika msafara huo wa kibiashara ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE
Kiwanda Cha dawa Cha Kairuki Pharmaceutical industry LTD(KPIL) kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika Kwa kuwapatia Maji tiba (Drips) na Dawa za maji wanazozitengeneza katika Kiwanda hicho kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kuendelea kutanua wigo wa sekta ya Afya katika Mataifa hayo.
Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda Cha dawa Cha Kairuki Pharmaceutical industry LTD(KPIL) Bw. Benson Meikoki ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa majumuisho ya safari yao ya kibiashara ya wajumbe wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba. Amesema kuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho walipata fursa ya kushiriki msafara wa kibiashara baina ya nchi ya Tanzania na Sudan Kusini ambapo walikuwa na wadau wa sekta ya Afya, Kilimo, Elimu na wajasiriamali ili kujadili namna gani Tanzania itaweza kushirikiana na nchi ya Sudan Kusini katika sekta hizo.
Amesema Kiwanda Cha Madawa cha Kairuki(KPIL) ndio kilipewa dhamana ya kunadi sera zake kama mwakilishi wa Viwanda vya dawa Tanzania ambapo alielezea Masuala mbalimbali , awali alielezea Mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) ikiwa ni pamoja na hospitali ya Kairuki ambayo imekuwa ikiendelea kuwa hospitali bora nchini toka mwaka 1987.
Aidha amesema kuwa katika Hospitali hiyo kumekuwa na mafanikio makubwa kwani pia wamefungua kituo cha Upandikizaji Mimba (Kairuki IVF) kilichopo Bunju mazizini ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kupitia Wataalamu waliobobea kama vile Dkt. Clementina Kairuki na hivyo kuepusha gharama za safari za kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hiyo.
“Kupitia Mkutano huu tuliweza kueleza kuwa kwa sasa Afrika haiwezekani kutokuwa na mtoto bali anapatikana KAIRUKI IVF alisema Meikoki, pamoja na mambo mengine alisema mtandao huo wa KHEN una chuo kikuu cha madaktari , na chuo cha manesi.
Meneja Huyo ameendelea kusema Kiwanda Cha Kairuki kimeweza kutengeneza na kuzalisha chupa Millioni 60 Kwa Mwaka lakini pia kuajiri wafanyakazi zaidi ya 500.
Amesema miongoni mwa dawa mbalimbali ambazo zinazalishwa katika Kiwanda hicho ni pamoja Ringer Lactate,Mannitol, Paracetamol, Fluconazole, Ciprofloxacin, Sodium chloride 3%, DNS, NS, D5, D10, D50, na nyingine nyingi.
Amesema pia wanafanya Biashara na wadau mbalimbali zikiwemo za ndani kama vile MSD Tanzania bara, CMS zanzibar visiwani, na mahospitali kama vile Muhimbili, Lugalo, Rabininsia, TMJ na nyingine na biashara za nje kama vile Malawi, Zambia, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Yemen, pamoja na nchi nyingine ambazo wapo kwenye hatua za mwisho za makubaliano.
Aidha ameeleza lengo na madhumuni ya Kiwanda hicho ni kuweza kuzihudumia nchi za SADC kwani katika safari hiyo wamefanya mazungumzo na Sudan kusini ili kuangalia uwezekanao wa kufanya biashara na kupeleka madawa katika nchi hiyo.
Amesema kuwa safari iliyokuwa imeandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Baishara Tanzania TANTRADE imeleta fursa kwa kiwanda hicho kuweza kushirikia na nchi za Afrika.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment