BANCABC KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKUBWA | Tarimo Blog

Benki ya BancABC Tanzania, ambayo ni Kampuni tanzu ya Atlas Mara imesema itaendelea kuwekeza kwenye bidhaa na huduma bunifu ili kuendana na hali halisi ya maisha ya kila ya wateja wake. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

BancABC Tanzania iliandaa futari hiyo ambayo ilileta watu Zaidi ya 300 na kuongozwa na Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar ambaye alitoa wito kwa Watanzania wote bila ya kujali dini zao kuonyesha Umoja na mshikamano wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

‘Tumeandaa futari hii ili kuonyesha Umoja na vile tunavyowajali wateja wetu’, alisema Iman huku akisema kuwa benki hiyo imekuwa na utamanduni wa muda mrefu wa kuandaa futari ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

‘Tumekuwa na utamanduni wa kuandaa futari kila mwaka kama ishara ya kuonyesha upendo kwa wateja wetu kama ishara ya kuonyesha upendo na uaminifu wao kwa kuchangua sisi kama benki yao’, alisema Imani huku akiongeza kuwa matukio kama haya ya futari ni muhimu kwani pia ni muda muafaka wa kuongea na wateja na kujua mahitaji yao’.

Akizungumzia kuhusu bidhaa na huduma ambazo utolewa na benki hiyo, Imani alisema ‘Sisi BancABC tumekuwa tukitoa huduma na bidhaa ambazo zinanguza Watanzania wa kanda zote kama vile wateja binafsi, wajasiriamali wadogo na wakubwa pamoja na wateja wakubwa ambazo ni huduma za kuweka na kutoa fedha pamoja na mikopo nafuu.

‘Huduma na bidhaa zetu hizi ni za ubunifu wa hali ya juu na kutaendelea kuwekeza kwenye ubunifu ili kuendana na hali halisi ya maisha ya kila Mtanzania’, alisema Imani.

Imani aliongeza kuwa BancABC imejikita kwenye huduma za kimtandao “kidijitali” ili kuwezesha Watanzania wengi walio nje na ndani ya nchi kuendelea kufanya miamala na kukuza pato la Taifa. Alitaja baadhi ya huduma hizo ni Pamoja na kadi za malipo ya awali “pre-paid

card” kwa sarafu tano tofauti ikiwemo TZS, USD, GBP, EUR na Yuan ya Uchina, huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi yani “Mobile Banking”.

Huduma zingine ni huduma za kibenki kwa njia ya Internet yani Internet Banking ambapo mteja anaweza kufanya muamala na kutizama salio lake akiwa nyumbani au ofisini kwake kwa usalama kabisa, Malipo ya Serikali kwa njia za kimtandao yaani GEPG pamoja na huduma za kifedha kwa njia za Mawakala maarufu kama Agency Banking

Kwa upande wake, Kaimu Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar aliipongeza BancABC Tanzania kwa kuandaa futari huku akisema ni ishara ya kuonyesha upendo kwa jamii ya Waislamu. ‘Kuandaa futari hii sio tu kuonyesha upendo kwa wateja wenu lakini pia ni ishara ya upendo kwa jamii ya waislamu wote na vizuri kwani waislamu kwenye mwezi Mtukufu kuandaliwa futari ni ishara ya upendo na kuthaminiwa’, alisema Sheikh Omar huku akitoa wito kwa Watanzania wote bila kujali dini zao kuendelea kuonyesha Umoja na mshikamano na hasa kwa kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

‘Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru BancABC Tanzania kwa kuweza kuunga mkono jamii yetu na sana sana kwa jamii yenye ulemavu kwani ni mfano kuwa benki hii imejikita kwenye kuguza maisha ya kila Mtanzania.

‘Ni kawaida kwa mashirika ya kifedha kuwekeza sehemu ambayo wana uhakika wa kurundisha faida. Lakini BancABC imeonyesha utofauti kwani imeenda hatua mbele na kwa kweli huu ni mfano wa kupongezwa’, alisema Omar huku pia akiipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuunga mkono miradi ya maendeleo na hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.



Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar (kulia) naMkurungezi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John wakiwaongoza wateja na wafanyakaziwa benki ya BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaammwishoni mwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambaowako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kulia) akimkabidhi zawadi kwaKaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar wakati wa futariiliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurungezi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kushoto) na Mwenyekiti wa CCMMkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtevu (kulia) wakiwaongoza wateja na wafanyakazi wa benkiya BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishonimwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambao wako kwenyemfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar akiwaongozawateja na wafanyakazi wa BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijiniDar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwawale ambao wako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kulia) akimkabidhi zawadi kwaKaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar wakati wa futariiliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2