Baadhi ya Watoto yatima waliohudhuria Iftar hiyo.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye hafla ya Iftar iliyofanyika Kibaha nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani jana usiku Aprili 12, 2023.Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza kwenye Iftar hiyo hafla iliyofanyika Aprili 12 , 2023 nyumbani kwake Kibaha Mkoani Pwani.
Kutoka kushoto ni Afisa Habari Mkoa Nasra Mondwe na Khadija Kalili (Mwandishi Michuzi Media) wakiwa kwenye foleni ya kupata Iftar.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akiwa na katika picha ya Pamoja na baadhi yaWaandiahi wa Habari waliohudhuria hafla hiyo ya iftar
Khadija Kalili, Pwani
RAIS Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuandaa ftari kwa wajane na yatima walioko Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Dkt.Kikwete amesema hayo jana usiku Aprili 12 mwaka 2023 alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Iftar iliyoandaliwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuongozwa na RC Alhaji Abubakari Kunenge.
"Nasema dhahiri kwamba haikuwa chaguo kwa Watoto hawa kukosa wazazi wao bali ni mipango ya Mungu na kina mama wajane kupoteza waume zao lakini kwa ajili ya watu wema na wacha Mungu walioamua kuwakumbuka kuwafturisha leo tumekutana hapa kupata ftari pamoja nao hii ni ishara ya upendo wa hali ya juu,niseme tu sisi wengine tumekuja kukuunga mkono RC Kunenge katokana na jambo hili kubwa la ibada la kukumbuka yatima umefanya kama jinsi ulivyosema kuwa Iftar hii imeandaliwa na Mheshimiwa Rais wetu Kipenzi chetu Dkt.Samia Suluhu Hassan, tunamshkuru sana kwa moyo wake wa upendo, ukarimu na kuwakumbuka watoto yatima na wajane,amesema Dkt. Kikwete.
"Rais ana mambo mengi ya kufanya ikiwamo pamoja na kulitumikia taifa lakini ameweza kukumbuka kufanya ibada ya kufturusha kundi hili muhimu katika jamii nampongeza sana" amesema Dkt.Kikwete.
Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea kwa Mwenyezi Mungu amjaalie afya njema Rais Samia umri mrefu ili aendelee kuliongoza Taifa la Tanzania kwa amani na utulivu huku akizitatua changamoto za wananchi kwa hekima ya hali ya juu.
Aidha Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Kikwete amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Kunenge kwa kuongoza vema Mkoa wa Pwani kutokana na jinsi anavyojali maslahi mapana ya wananchi wa Mkoa huu, ikiwa ni pamoja na kujali maendeleo ya wananchi huku akimuombea dua Mwenyeezi Mungu amuwezeshe kumpa uwezo wa kimwili na kiakili ili aweze kutimiza yote mema aliyodhamiria kuyatenda kwa wan Pwani na mwisho amemshkuru kwa mualiko wa Iftar hiyo.
RC Kunenge akizungumza kwenye Iftar hiyo amesema kwa kuwaeleza wakaazi wote wa Pwani kutumia vema fursa zilizopo ndani ya Mkoa hasa Viwanda na Biashara katika kujiletea maendeleo.
"Kila mtu awe mchungaji wa mwenzake katika jamii na hili ni jukumu la wote kwani hasa hivi sasa Dunia imegubikwa na utanda wazi na janga la maadili yanayokwenda kinyume na maadili ya dini pamoja na mila zetu hata katika vitabu vitakatifu vimepinga ikiwemo,Torati,Zaburi,Injili na Qur'ani tuwalinde watoto wetu ili kesho kwa Mwenyeezi Mungu tukapate maskani mema kwa sababu tukishindwa kukilinda kizazi chetu tutakwenda kuulizwa kwa Mola wetu" amesema RC Kunenge.
Iftar hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Serikalini wakiwemo Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Wakurugenzi na Viongozi kutoka katika madhehebu mbalimbali ya dini,viongozi wa Vyama vya siasa ikiwemo Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kamati ya Ulinzi na UsalamaMkoa wa Pwani , Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani pamoja watu binafsi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment