Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea HESLB jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (mwenye miwani) akizungumza wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula alipotembelea HESLB jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea HESLB jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya HESLB wakati alipotembelea jijini Dar es Salaam.
*Badru:tunaendelea kutoa elimu ya urejeshaji wa mikopo kwa wanufaika.
Na Chalila Kibuda , Michuzi Tv
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amesema kuwa ni muhimu kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga katika utoaji wa mikopo kutokana na mageuzi ya kuhamasisha elimu ya ufundi na ujuzi.
Dkt. Rwezimula ameyasema hayo wakati alipotembelea ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa HESLB inatekeleza majukumu mengi katika utoaji wa mikopo na kuhimiza taasisi hiyo ya kugharamia elimu ya juu kuendelea kutoa elimu ya kuongeza uelewa wa masuala ya utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa wanufaika.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa katika siku zijazo suala la elimu litazingatia zaidi ujuzi na hivyo HESLB inatakiwa kwenda kusaidia eneo hilo na kuweza kupata wataalam wenye ujuzi na wenye ushindani katika soko la ajira.
“Baadhi ya waajiri wanaajiri wenye Stashahada na Astashada hivyo katika mwelekeo wanatafuta ujuzi na ndio Serikali imetazama katika eneo”amesema Dkt.Rwezimula
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema kuwa utaratibu wa utoaji wa mikopo umewekewa utaratibu wa nani anatakiwa kupata kutokana na maelezo ya maombi na juu ya uhitaji wa mkopo huo.
Amesema kuwa Bodi inaendelea na kutoa elimu ya urejeshaji wa mikopo kwa walionufaika kwa kuwa mikopo hiyo inakwenda kusaidia wahitaji wengine.
Katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Franklin Rwezimula aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala –Taasisi ikiwa ni kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na Bodi katika utoaji wa huduma kwa watanzania katika eneo la upataji mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment