MASALA PRINCESS KUSHIRIKI LIGI YA DARAJA LA KWANZA | Tarimo Blog



Timu ya wanawake ya Masala Princess inayoshiriki ligi ya Daraja la kwanza kwa wanawake Tanzania Bara inatarajia kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya kushiriki mashindao hayo. Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza tareh 12 hadi 25 Aprili mwaka 2023 katika viwanja vya shule ya Alliance jijini Mwanza.

Akizungumza Meneja wa timu hiyo Ester Mpanda timu ya Masala Princess imejipanga vizuri kushiriki kwenye ligi hiyo na wanaamini watakuwa washindi na kupanda ligi kuu ya Wanawake ya Srengeti Lite(SWPL) kwa msimu wa 2023/2024.

Pia amesema kwa taaarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) wanaoruhusiwa kucheza ligi hiyo ni wale ambao hawajasajiliwa kucheza Ligi kuu ya Wanawake msimu wa 2022/2023 na ambao usajili wao utakuwa umetishwa na Shirikisho hilo.

Mpanda amewaomba wadau mbalimbali yakiwemo makampuni au taasisi yoyote kuweza kujitokeza kutoa msaada kwa timu hiyo ili vijana waamasike kwenye mashindano hayo na pia ameishukuru kampuni ya Abec kwa kuendelea kuidhamini timu ya Masala Princess.

Timu 16 zinatarajiwa kushiriki ligi hiyo ambazo ni Bilo FC kutoka Mwanza, TSC Queens kutoka Mwanza, Ukerewe Queens kutoka Mwanza, Bunda Queens kutoka Mara, Geita Gold Queens kutoka Geita, Singida Warriors ktoka Singida, Allan Queens kutoka Singida, Mt. Hanang Queens kutoka Manyara, Lengo Queens kutoka Arusha, Mlandizi Queens kutoka Pwani, Ilala Queens kutoka Dar es Salaam, JMK Park Queens kutoka Dar es Salaam, Masala Princess kutoka Dar es Salaam, Oysterbay Queens kutoka Dar es Salaam, Ruangwa Queens kutoka Lindi na Mapinduzi Queens kutoka Njombe na timu zote zitaripoti tarehe 10 Aprili, 2023.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2