Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kutoa Futari kwenye Jamii Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ndugu Ahmed Missanga ameungana na Waumini Mbalimbali katika Msikiti Mkuu wa Sepuka Wilayani Ikungi katika kutoa Iftari na Dua Maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi mbalimbali wa Mkoa Singida.Kabla ya Dua hiyo comrade Missanga pamoja na taasisi ya Faraja trust fund pamoja na sheikh wa Mkoa wa Singida walitembelea Gereza Kuu la Singida na kuwapelekea Wafungwa sadaka ya Futari na mahitaji mbalimbali.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ndugu Ahmed Missanga anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini na Mkoa wa Singida Ramadhani njema.
Kwa upande wake Imamu wa Msikiti wa Sepuka Sheikh Jumanne Mohamedi Mughenyi pamoja na Imamu wa Msikiti wa Mwaru sheikh Omari Mgisa na Imamu wa Msikiti wa Irisia sheikh Jumanne Kungu wamemshukuru sana Kiongozi huyo kwa kutoa iftar katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan na mawaidha aliyoyatoa kuhusu kuwalinda Vijana dhidi ya vitendo vya mmomonyoko wa Maadili na kuwataka Wazazi kuendelea kukemea vitendo vinavyohatarisha ukiukwaji wa Maadili ya Mwafrika..jpeg)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

.jpeg)
.jpeg)

Post a Comment