TTCL 'WALA' PASAKA NA WATOTO YATIMA JIJINI DAR | Tarimo Blog

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Adeline Berchimance (kulia) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home', Bw. Kondo Kondo (wa pili kulia) mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home' kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Maofisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL (mbele) wakiimba pamoja na watoto wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home' mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wa Kituo hicho kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Maofisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL (mbele) wakijumuika pamoja na watoto wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home' mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wa Kituo hicho kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Maofisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL (mbele) wakiwa na Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home', Bw. Kondo Kondo (katikati waliosimama mbele) katika picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home' mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wa Kituo hicho.

Baadhi ya watoto wa Kituo cha 'Daniel Brother Center'maarufu kama Dogodogo Center - Bunju cha jijini Dar es Salaam wakishiriki kushusha msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wanaoishi katika kituo hicho.

Baadhi ya watoto wa Kituo cha 'Daniel Brother Center'maarufu kama Dogodogo Center - Bunju cha jijini Dar es Salaam wakishiriki kushusha msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wanaoishi katika kituo hicho.

Sehemu ya msaada wa vyakula na vinywaji vilivyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wa Kituo cha 'Daniel Brother Center'maarufu kama Dogodogo Center - Bunju jijini Dar es Salaam jana.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Adeline Berchimance (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Kituo cha 'Daniel Brother Center' maarufu kama Dogodogo Center - Bunju, kwa ajili ya kutoa msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto Kituo hicho, kushoto ni mwenyeji wake na Mkuu wa Kituo, Fr. Dk. Dyering Maliti.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Adeline Berchimance (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa Mkuu wa Kituo cha 'Daniel Brother Center' maarufu kama Dogodogo Center - Bunju, Fr. Dk. Dyering Maliti.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa msaada wa vyakula pamoja na vinywaji vya Siku Kuu ya Pasaka kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima na waliopo katika mazingira magumu.

Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni Kituo cha 'New Life Orphanas Home' na Kituo cha 'Daniel Brother Center'maarufu kama Dogodogo Center - Bunju vyote vikiwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza akikabidhi msaada huo jana, Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga, alisema jukumu la kuwasaidia watoto yatima na walio katika mazingira magumu ni la jamii nzima hivyo kutoa hamasa kwa kila mwenye uwezo na nafasi kushiriki katika kuwasaidia watoto hao.

Alisema jamii ha ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa jamii kusapoti, amewashukuru viongozi wa vituo hivyo kwa moyo wa upendo wanaouonesha kwa watoto hivyo kuzitaka taasisi, mashirika na jamii yote kuwaunga mkono kwa kusaidia baadhi ya changamoto kwenye vituo anuai vya yatima na watoto walioko kwenye mazingira magumu.

Hata hivyo katika hatua nyingine ameiomba jamii kubadilika kwa kuzingatia maadili na kuwa na upendo kwa kila mmoja na familia kuwajibika kwenye suala zima la malezi ili kupunguza watoto wanaokimbilia mitaani. 

"Chanzo cha watoto wa mitaani au watoto kukimbilia mitaani kinatokana na wanajamii wote, hivyo endapo kila mmoja atawajibika katika malezi ya watoto tutapunguza kiasi kikubwa hili suala la watoto kukimbilia mtaani au kwenye vituo vya kuwalea," alisema Bi. Berchimance.

Hata hivyo, aliitaka jamii kuliunga mkono Shirika la TTCL hasa katika huduma mpya ya intaneti ya kasi zaidi kutoka TTCL maarufu kama Faiba mlangoni kwako yanayompa fursa mteja kuperuzi bila kukwama huduma ya intaneti yenye kasi zaidi nchini. #RudiNyumbaniKumenoga.

Kwa upande wao Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha 'New Life Orphanas Home', Bw. Kondo Kondo ambaye kituo chake kina jumla ya watoto 105 na Mkuu wa Kituo cha 'Daniel Brother Center' Dogodogo - Bunju, Fr. Dk. Dyering Maliti chenye watoto 76 wamemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga pamoja na wafanyakazi wote kwa kuonesha moyo wa upendo kwa watoto wahitaji katika vituo hivyo na kuiomba jamii kuungana pamoja kusaidia.

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2