Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Kenneth Hoseah na Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu jijini Dar es Salaam Aprili 04, 2023.
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 04, 2023 mara baada ya uzinduzi wa Kitabu kilichoandikwa chini ya mradi wa ’Ushirikiano Mpya katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).
Stefano Ponte kutoka Shule Kuu ya Biashara ya Copenhagen akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 04, 2023 mara baada ya uzinduzi wa Kitabu kilichoandikwa chini ya mradi wa ’Ushirikiano Mpya katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).
Dan Brockington kutoka Chuo Kikuu cha Autonomous Barcelona akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 04, 2023 mara baada ya uzinduzi wa Kitabu kilichoandikwa chini ya mradi wa ’Ushirikiano Mpya katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Kenneth Hoseah akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kitabu kilichoandikwa chini ya mradi wa ’Ushirikiano Mpya katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Anangisye
Matukio mbalimbali.
CHUO Kikuu cha Dar ea Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii wamezindua kitabu kuhutimisha mradi wa ’Ushirikiano wawadau mbalimbali katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 04, 2023 mara baada ya uzinduzi wa Kitabu hicho, amesema kuwa utafiti wao ulijikita kwenye Maliasili, Misitu na Mazao ya bahari.
“Kwahiyo tumeangalia upande wa jamii zinazopatikana karibu na Misitu, kitabu kimesheheni mambo mhimu ya jamii na namna inavyofaidika uwepo wa maliasili zinazowazunguka pamoja na changamoto wanazokutana nazo.” Amesema Prof. Christine
Ameomba jamii zifikiwe na tafiti hizo ili kuweza kubadilisha hali ya kiuchumi za wananchi wanaozungukwa na maliasili husika mahali walipo.
"Machapisho ya kitaaluma tumefanya sasa yapo kwenye sehemu zinazotakiwa za kitaaluma lakini mapendekezo ya serikali nini ifanye, tulitafuta wadau wa maliasili, wakurugenzi wa maliasili, wa misitu na Uvuvi tukajadiliana nakuja na machapisho madogo ya kisera ili serikali uweze kubadilisha sera kulingana na maisha ya sasa". Ameeleza
Kwa upande wa wahariri wa kitabu hicho Dan Brockington kutoka Chuo Kikuu cha Autonomous Barcelona amesema kuwa walifanya utafiti huo kwa ushirikiano mkubwa kati yao na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Tanzania inabahati ya kuwa na watafiti wengi wanaofanya kazi zao katika usimamizi wa maliasili kwahiyo imekuwa ni rahisi kwao kufanya utafiti huo juu ya misingi mizuri ambayo ilikuwa imejengwa tayari." Amesema Brockington
Amesema changamoto kubwa ni kulinganisha chanzo cha mapato kwa wananchi ni tofauti na maliasili inayopatikana katika eneo husika.
Amesema kuwa kama eneo la hifadhi ya maliasili imeongeza basi na kipato cha wananchi kiwe kizuri.
Kwa upande wa Stefano Ponte kutoka Shule Kuu ya Biashara ya Copenhagen, amesema kuwa ushirikiano katika utafiti huo ulianza 2016 hadi 2020 ingawa yeye alikuwa na mawazo mengine katika utafiti huo.
Amesema waliungana pamoja katika utafiti huo na sasa wanasheherekea uzinduzi wa kitabu hicho pamoja hii ni hatua kubwa kwani hata yeye amesema amejifunza kupitia utafiti huo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment