Na Elias Gamaya, Michuzi TV Shinyanga.
Wakazi Zaidi ya 30,000 wa kata tatu zaUlowa, Ubagwe na Ulewe zilizo ndani ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga wamekosa huduma za mawasiliano ya barabara kwa siku kadhaa baada ya mvua kubwa kunyesha na kuharibu daraja la mto Ubagwe.
Wakazi wa Ene hilo wanasema wanapata adha kubwa ya Kuvuka Katika Daraja Hilo ambapo wengine hutozwa Shilingi Elfu 5000 Kwa ajili Ya Kuvushwa.
Diwani wa kata ya Ulowa Gabriela Kimaro ameiomba serikali kuchukua hatua za haraka ili wananchi waweze kuondokana na adha hiyo,huku mbunge wa jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani akiomba wakala wa barabara Tanzania mkoa wa shinyanga (TANROD) kuchukua hatua za haraka kiokoa wakazi wa kata hizo tatu
Kwa upande wake Mhandisi Hans Kipamila Kaimu meneja wa TANROAD mkoa wa Shinyanga amesema watafanya tathmini changamoto hiyo na kuiwasilisha sehemu husika ili kufanya marekebisho ya barabara hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment