Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesitisha mikopo kwa walimu Wanafunzi wanne waliomshambulia na kumdhuru Mwanafunzi wa Mbeya kutwa sekondari. Bodi imechukua hatua hiyo baada ya wanafunzi hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu katika taasisi walizokuwa wanasoma.Bodi iliendelea kuidhinisha kwamba imechukua hatua hiyo baada ya wanafunzi hao kuonesha utovu wa nidhamu na na hivyo kusimamishwa masomo, kitendo cha kusimamishwa masomo kimewafanya walimu wanafunzi hao kupoteza sifa za kuendelea kupokea mkopo.
Pia ilieleza kwamba, walimu wanafunzi hao watapaswa kurudisha kiwango chote cha fedha ambacho walikopeshwa. Bodi imewataja Walimu hao ambao walikuwa katika mafunzo ya vitendo nao ni;-
1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
Kwa taarifa zaidi tembelea hii link hapa chini
Duuu Tanzania yetu
ReplyDeleteHÃ tar
ReplyDeleteInabidi tuende nayo hivyo hivyo Mr Sinkala
ReplyDeletePost a Comment