KUTOKA WIZARA YA ELIMU-UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA

Leo tarehe 18 Oktoba, Wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia imetangazia viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.
Imetangazwa kwamba uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, ambapo vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.
Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, imetangazwa kwamba, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.
Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.
Tangazo hili limetolewa na
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Hii hapa link ya tangazo hili kwa uhakika zaidi
http://moe.go.tz/sw/component/k2/item/504-taarifa-kwa-umma-kuhusu-uhakiki-wa-vyuo-na-wanafunzi-wanaoendelea-na-masomo-ya-shahada
 

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2