TANGAZO LA UFADHILI WA MASOMO YA ASTASHAHADA/CHETI NA STASHAHADA KUTOKA WIZARA YA AFYA

Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto imetangaza kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa kada ya afya katika ngazi ya astashahada/cheti na stashahada katika vyuo vya serikali, ambao hawana
uwezo wa kugharamia masomo yao ambao wako tayari kufanya kazi katika mikoa na halmashauri ambazo zina uhaba mkubwa wa watumishi.
Ufadhili huu utawahusu wadahiliwa wote wa masomoya Astashahada/cheti na stashahada katika mwaka wa masomo 2016/2017 katika vyuo vya serikali.
Waombaji wa ufadhili huu wanapaswa kutimiza masharti yafuatayo:
  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe amedahiliwa kusomea mojawapo ya fani katika kada ya afya katika chuo cha serikali kupitia mfumo wa pamoja wa kudahili (CAS).
  3. Kada zilizoainishwa katika ufadhili huu ni Uuguzi na ukunga,tabibu na tabibu msaidizi,maabara na famasia.
  4.  Awe tayari kuingia mkataba na serikali wa kufanya kazi katika mikoa na halmashauri ambazo zina uhaba wa watumishi.
  5. Awe tayari kutii masharti ya mkataba atakaoingia na serikali.
Waombaji wanapaswa kutuma maombi yao kwa barua kwa Mkuu wa chuo walichochaguliwa wakibainisha bayana Halmashauri atakayopenda kufanya kazi baada ya kuhitimu mafunzo yake. baada ya kuwasilisha maombi hayo, atapewa mkataba ambao ataujaza na kuurudisha kwa mkuu wa chuo ambae ataupeleka wizarani kwa hatua zaidi.
Mwisho wa kupokea maombi vyuoni ni tarehe 11 November 2016
 Bofya hapa kulipata Tangazo hili kwa undani zaidi

1/Post a Comment/Comments

  1. Nice,iam looking for scholarship,study's in Tanzania. If there is any sponsores please help me .

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2