SERIKALI YATANGAZA AJIRA KWA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA SHULE ZA SEKONDARI

Serikali inatarajia kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari.
Ajira hii ni kwa walimu wa stashahada na shahada za mafunzo ya ualimu wa masomo ya hisabati na sayansi, waliohitimu mwaka 2015.  wahitimu hao wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya elimu ya sekondari (kidato cha nne na sita) na taaluma ya ualimu (stashahada na shahada) kwa ajili ya uhakiki.
Nakala hizo ziwasilishwe kupitia barua pepe ya wizara info@moe.go.tz kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi ijumaa tarehe 16/12/2016.
yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika uajiri.
Tangazo hili linapatikana pia kwenye tovuti za ofisi zifuatazo: OR-TAMISEMI, NECTA, TCU na NACTE.
imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2