Mkongwe
wa Filamu za Kibongo nchini, aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza
vichekesho, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, aliyeanza kuagiza mwaka 1958
akiwa na miaka 10, ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji
na kumrudia Mungu, amesema ataendelea kuigiza hadi anakufa kwa sababu
uigizaji upo kwenye damu na hii inadhihirishwa wazi kwani ni miaka 58
sasa ya uigizaji wake na fani hii ameianza akiwa darasa la pili.
Majuto
alizungumza hayo Dar es salaam Jana.Alisema hawezi kukubali kuona fani
inachezewa na watoto, hivyo ataendelea kuigiza hadi siku atakayokufa kwa
sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.
”Kuigiza
kwangu ni kama maradhi vile, hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi
kukaa pembeni sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa,
nitaendelea kuigiza hadi nakufa,” alisema Majuto.
Mzee
Majuto aliongeza ataendelea kuigiza ili kuhakikisha anapata chipukizi
ambaye anaweza kufanya kile alichokuwa anakifanya yeye hapo baadae.
Alisema
bado hajapata mtu wa kurithi mambo yake katika tasnia hiyo, hivyo
hawezi akakurupuka kuachana na kazi hiyo bila ya faida ambayo kwa upande
wake ni kupata mrithi.
Post a Comment