1. Awe mwema
2. Mwenye hekima
3. Mwenye adabu
4. Mwenye busara
5. Awe mkarimu
6. Msafi (mwili na nyumba)
7. Mpole
8. Mwenye huruma
9. Mdadisi
10. Mvumilivu
11. Mcheshi (kiasi)Yampasa mke aanze siku kwa kauli nzuri hata kama anaumwa:--
Amsalimie mume
- Amwage mumewe akimtakia kazi njema
baada ya kumuandalia
(a) Maji ya kuoga
(b) Kifungua kinywa
(c) Nguo za kuvaa siku hiyo
Mume atokapo kazini:-
(a) Mkaribishe kwa tabasamu, mkaribishe
kwa furaha.
(b) Mpigipige mgongoni
(c) Vaa nguo nzuri (mwanaume hupendaanachoona) macho huvutiwa kwa kuona
(d) Waeleze watoto wako unavyompendababa yao ( watoto nao watawapenda wote)
(e) Kila mmoja wenu ajue kile anachopenda ua anachotaka
ILI KUMHESHIMU MUME
1. Muombee kila siku - Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi, uelewa,
kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk -
angalia na tarajia majibu ya maombi - Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa
familia yako - Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako- ombea mtazamo wako.
2. Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
3. Angalia sifa za mumeo na uzikubali na ongeza mara kwa mara
4. Mwambie mumeo ni namna gani unamfurahia na kumpenda
5. Usitoe sifa zake mbaya mbele za watu au kubisha
6. Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumuJihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
7. Changamkia pale anapoonesha upendo
8. Fikiria mambo mazuri juu ya mumeo
9. Thamini vitu anavyovipenda na asivyovipenda Mith 12:4
KAWAIDA MWANAMKE
1. Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako
2. Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye.
3. Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko
4. Utampa mume wako haki yake
5. Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote.
6. Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu
7. Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu ( siri za ndani zisitoke nje)
8. Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
9. Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba
10. Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine
11. Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupednekeza njia ya kupita na siyo kunyang'anya usukani
SIFA ZA MWANAUME
1. Mpole
2. Asiwe mwepesi wa hasira
3. Mcheshi
4. Anayeshaurika
5. Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
6. Aliye na shukurani na kusifu (kwa lolote jema alilolitenda mkewe)
7. Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote.
WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE
1. KUPENDA - matatizo mengi hutokea kwa sababu watu hawajui maana na jinsi ya kupenda kupenda ni matendo (action) siyo
kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA
- Mume ni kichwa cha mke
MLINZI WA MKEWE
- Mke hujiona salama awapo na mumewe.
Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa
ndani na nje kama vile baba na mama,
mashemeji/mawifi na marafik
4. KUTUNZA FAMILIA.
Kuhakiki familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto
KUMPAMBA MKEWE - mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze
kuvutia (amununulie vipodozi, nguo nk)
KAWAIDA MWANAUME:
1. Utamheshimu mke wako kama mrithi
2. Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako
4. Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako
5. Utaendelea kumpenda kwa upendo ule
wa kwanza wa wakati unampata.
6. Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako.
7. Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya
8. Macho yako yataelekea kwa mke wako tu
na sivinginevyo.
9. Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako.
10. Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo.
11. Hutakuwa mchungu likija swala la fedha.
WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE KUTII
- Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi,basi mke atatii
uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali
KULEA WATOTO (FAMILIA)
(a) Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
(b) Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
(c) Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
(d) Kufundisha watoto maneno ya Mungu
(e) Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.
KUMSHAURI MUMEO
Mke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe. Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi. Ushauri unafaa lakini ushauri
mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi.
ADUI WA NDOA NI:-
UTAJIRI - Tajiri hupendwa na wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mkewe
UMASKINI - kazi ya kutafuta lishe ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume
MADARAKA - madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbanini chukuzo kwa mume/mke.
Maafisa hawana muda na wake zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.- Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili- Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo
kusababisha mke kupinduliwa na house girl.
MAMBO YANAYOWAKERA WAKE
1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani..
Post a Comment