Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka watanzania kuendelea kumuombea dua pamoja na ushirikiano katika majukumu yake mpya. “Nimepokea salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza kumjibu kila mtu, uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele mlizotuombea, nawashukuru sana ndugu zangu.
Tuzidi kuombeana dua tu. Tuna kazi ngumu ya kukimbia kukidhi matarajio ya kiongozi wetu Mkuu aliyetuamini na matarajio ya wananchi wenzetu. Binafsi nawaahidi nyote kuwa sintowaangusha! Ahsanteni sana ndugu zangu, natarajia ushirikiano wenu wa kila hali.” Alieleza Dk. Hamisi Kigwangalla.
Awali taarifa za kuteuliwa kwake katika wizara nyingine, alizipata kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kwa njia ya simu wakati akiwa kwenye majukumu ya ziara ya kuboresha mfumo wa afya, akiwa Wilayani Nachingwea, Kata ya Kilimalondo umbali wa zaidi ya kilometa 100, kutoka Makao makuu ya Wilaya hiyo ya Nachingwea, aliweza kusitisha ziara yake hiyo ambayo alitakiwa kuendelea katika Vijiji na Wilaya nyingine ya Liwale.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Dk.Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya Kilimalondo wakati wa ziara hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment