Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi ameendeleza wito wake wa kuzitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ( OAG), Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OSG)na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameyasema hayo hivi karibuni katika mazungumzo yake mafupi na Mawakili wa Serikali wanaosimamia Ofisi hizo tatu katika Mkoa wa Tanga wakati akiwa Mkoani hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii katika mahojiano mafupi. Wakili wa Serikal Mwadamizi, Rebecca Msalanhi amesema. “Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Feleshi amesisitiza ushirikiano kati ya Ofisi hizi tatu na kututaka tufanye kazi kwa kushirikiana”.
Akaongeza pia kwamba, Mhe. AG pia amezitaka Ofisi hizo kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Taasisi nyingine zilizomo ndani ya mkoa huo kwa kutoa msaada wa kisheria pamoja na mambo mengine.
Aidha kwa mujibu wa Wakili Mwandamizi Rebecca Msalanhi , Mwanasheria Mkuu amemuagiza Mwakilishi huyo wa Mwanasheria Mkuu katika Mkoa wa Tanga kuanza mchakato wa kutafuta kiwanja katika Wilaya ya Mkinga.
Katika ziara hiyo ambayo ilijumuisha Uongozi wa Mahakama akiwamo Jaji Kiongozi Mhe. Mustapher Siyani, Makamishna Adv Julius Bundala Kalolo na Adv Genoveva Kato, pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga, walitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mahakama Mahakama ya Wilaya ya Mvomero .
Akiwa Mkoani Morogoro, Mhe. Mwanasheria Mkuu wa serikali alipewa heshima ya kupanda mti wa kumbukumbu katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
Ziara ya viongozi hao ilifanyika kati ya March 8 hadi 11 2022.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Eliezer Feleshi na Jaji Kiongozi Mhe. Mustepher Siyani wakiangalia michoro ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akipanda mti wa kumbukumbu katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima na Mawakili wa Serikali Rebecca Msalanhi Ofisi ya Mwanasheria Mku wa Serikali Tanga, Luciana Kikala Wakilli wa Serikali Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Tanga na Juma Maige Mwendesha Mashtaka wa Mkoa wa Tanga, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mhe. AG alikuwa Mkoani Tanga akiambatana na Viongozi wa Mahakama kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga mkoani humo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
OcornoZas-na1978 Stephanie Sims Crack
ReplyDeletesmugrereati
Post a Comment