TAASISI YA MWANAMKE USUKANI YAFANYA ZIARA YA KUWATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA MUHIMBILI-MOI NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI

IMG_6540

Baadhi ya Wanafunzi wa Taasisi ya Mwanamke kwenye Usukani ambao wamefanya ziara katika Hospitali ya Muhimbili Moi kwa ajili ya kutoa damu na misaada mbalimbali.

IMG_6547

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa  misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili jijini Dar es salaam

IMG_6544

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone wa kwanza kushoto akiwa na wanafunzi wake ambao wanasomea mambo ya udereva walipofanya Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa  misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili 

IMG_6554

Mwanafunzi kutoka Taasisi ya Mwanamke Usukani,Mary Kihanga akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) akielezea namna walivyoweza kujitolea kwa ajili ya kusaidia wagonjwa mbalimbali katika hospitali ya Muhimbili.

IMG_6563

Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Moi, Patrick Jonh akiishukuru Taasisi ya Mwanamke Usukani kwa kuweza kutoa misaada mbalimbali katika kitengo hicho .

IMG_6568

Wakitoa misaada katika vitanda vya wagonjwa ambao wamelazwa Muhimbili.

IMG_6571

Mwakilishi wa Polisi WP Saburi Chutto wa kwanza kushoto wakimsikiliza mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Muhimbili

IMG_6573

Wanafunzi toka Taasisi ya Mwanamke Usukaniwakisubiri kutoa damu kwa ajili ya wagojnwa mbalimbali katika Kitengo cha Moi

………………….

Taasisi ya tiba na mifupa Muhimbili MOI imewashukuru taasisi ya Wanawake Usukani  kwa kwenda kutoa misaada mbalimbali katika kitengo hicho ambacho ni muhimu kwa jamii .
Afisa uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Jonh amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipotembelewa na taasisi hiyo  kwenda kuchangia damu kwa wagonjwa wanaohitaji damu, kwani katika kitengo hichi kina uhitaji mkubwa wa damu ili waweze kusaidia wagonjwa.
Kupitia mkurugenzi wa kampuni ya Wanawake Usukani Martin Gabone ambae anendesha mradi wa kuwajengea wanawake uwezo amesema kuwa wamenda kutoa misaada hiyo kwani kupita taasisi hiyo wanawake wanafursa ya kujifunza udereva hivyo ni chachu hata wao pindi watakapopata ajali waweze kusaidiwa kama leo walivyofanya wao pia iwe kioo kwa watu wengine waweze kwenda kuchangia damu na kutoa misaada.
Aidha aliongeza kuwa jamii inabidi iondokane na dhana ya kwamba wanawake hawawezi kuamua jambo, kwani sasa kuna fursa nyingi ambazo wan awake wanaweza kujikomboa kiuchumi na hata kijamii.


SOMA ZAIDI

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2