Wataalam wa Afya Magugu wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha na watumishi wa kituo cha Afya Magugu wilayani Babati.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Magugu wilayani Babati.
……………….
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amemwagia sifa lukuki mbunge wa Jimbo la Babati vijiji Mkoani Manyara Jitu Son kwa uchapakazi wake na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.
Jafo amesema hayo aliposimama kituo cha Afya Magugu wilayani humo na kuwaona wagonjwa wa kituo hicho akitokea mkoani Kilimanjaro kikazi na kuelekea mkoani Dodoma.
Jafo amewapongeza sana watumishi wa kituo hicho cha afya kwa kujituma katika kuwahudumia wananchi wa Babati vijijini.
Alipokuwa akiwasalimia wagonjwa na kuongea na watumishi Waziri Jafo alisema ” Nyinyi watumishi na wananchi wa babati mmepata mbunge makini sana ambaye anawapigania muda wote.
Muungeni mkono mbunge wenu kwa kila hali kwani anapambana sana kwaajili yenu”.
Hata hivyo watumishi wa kituo hicho hawakusita kuiomba serikali iangalie uwezekano wa kituo hicho kufanyiwa ukarabati kama vinavyo boreshwa vituo vingine hapa nchini ili kukiwezesha kituo hicho kutoa huduma bora zaidi.
Akijibu ombi hilo,Waziri Jafo aliwajulisha watumishi hao kwamba amelichukua ombi hilo kwani hata mbunge wao alisha lifikisha katika Ofisi yake hivyo wataangalia fursa itakayojitokeza siku za usoni ili kukiboresha kituo hicho. Baada ya tukio hilo Waziri Jafo ameelekea wilayani Kondoa mkoani Dodoma kukagua miradi ya afya, barabara, na elimu.
SOMA ZAIDI
Post a Comment