KILA MWAKA WATANZANIA 50,000 HUPATA SARATANI

Zamototz
*Yaelezwa saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza 
*Wanafunzi wa kike kuanzia darasa la nne kupewa chanjo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road imesema imekuwa ikipokea wagonjwa wapya wa saratani 50,000 kila mwaka huku ikielezwa saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoonekana kuongeza.

Pamoja na hali hiyo, imeelezwa jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali kwa kushirikiana na taasisi hiyo ambapo wameweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wa kike waliopo kuanzia dasara la nne nchi kote watapatiwa chanjo itayakayosaidia kuwakinga na aina hiyo ya saratani.

Hayo yamesemwa leo (jana)  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Chrispin Kahesa wakati wa semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa satarani, hali ilivyo kwa sasa nchini, sababu zinazosababisha ugonjwa huo na pamoja na jitihada zinazochukuliwa kupunguza kasi ya saratani nchini.

WATANZANIA 50,000 KILA MWAKA HUPATA SARATANI

Akizungumzia ugonjwa huo ,Dk.Kahesa amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(HWO), Tanzania kila mwaka kunakuwa na wagonjwa wapya 50,000 wa saratani na hivyo unaweza kuona ukubwa wa ugonjwa huo nchini kwetu.

"Kila mwaka Tanzani wagonjwa wapya wa saratani ni 50,000.Ni idadi kubwa ambayo lazima tuweke mikakati ya pamoja kuhakiksha tunapunguza idadi hiyo na ukweli tunaweza."Ni suala la kuamua tu kuanzia mtu mmoja mmoja, familia na Watanzania kwa ujumla kwani baadhi ya sababu zinazosababisha ugonjwa huu tunaweza kuzikwepa.

"Baadhi ya sababu zinazosababisha saratani ni uvutaji sigara, pombe, vyakula vyenye mafuta mengi, kutofanya mazoezi ya mwili,unene na  taka sumu.Hivyo ukiangalia hizo sababu unaweza kuziepuka na ukishindwa zote basi chagua hata sababu mbili zieupuke,"amesema.

Amefafanua zipo saratani ambayo hutokana na kirusi ambacho hubebwa na mwanaume na kisha kukiacha kwa mwanamke kupita tendo la ndoa na aina hiyo ya kirusi ndicho kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi.




from Michuzi Blog
Soma Zaidi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2