MADARASA YA NYASI, TEMBE, UDONGO YASITUMIKE KATIKA SHULE ZOTE NCHINI-WAZIRI JAFO

Zamototz
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.

“Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari kusoma”Alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi  kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini.

Niwapongeze baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akifungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakugenzi wa Halmashauri yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi yanayofanyika kwa siku Tano Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kufungua mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja akiwasilisha taarifa ya Utangulizi wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
Mkuu wa Wilaya ya Londido Mhe. Daniel Chongolo (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe wakati wa mafunzo ya Uongozi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


from Michuzi Blog
Soma Zaidi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2