Na Magreth Kinabo .
JAJI Mkuuwa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema kwa Kituo cha Mafunzo na Habari cha Mahakama kilichopo katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam kitasaidia kuboresha utendaji kazi kwa Watumishi wa Mahakama na wadau wake.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu huyo wakati alipozindua kituo hicho , ambapo alisema kitakuwa ni sehemu ya mafunzo ya kuweza kuendelea kuwajengea uwezo watumishi hao na wadau Mahakama ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha wa masuala mbalimbali ya kisheria .
Aliongeza kwamba kituo hicho, kielelezo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) hivyo kinaweza kusaidia watumishi wa Mahakama kutenda haki kwa wakati, ikiwemo na kupata habari.
“Kituo hiki kitasaidia jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu ya mafunzo ya kisheria, kwa kuwa kitatoa mafunzo ya kisheria ili kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama kuwa na uelewa wa kutosha katika masuala ya Kielektroniki na kwenye maeneo mapya ya kisheria ,” alisema Juma.
Profesa Juma alifafanua maeneo hayao kuwa ni masuala ya kisheria ya mtandao, dawa za kulevya hivyo kinaweza kubaini kuwa mtu akifanya kosa anaweza kufungwa au kama ana hatia kuachiwa.
Aliwataka watumiaji wa kituo hicho, kuhakikisha kinakuwa na habari muhimu kwa maendeleo ya nchi ilinganishwa na nchi nyingine ili kuifanya Tanzania inakuwa inafanya vizuri kuhusu utekelezaji wa mikataba na ubora wa ufanyaji biashara.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mkazi kutoka Benki ya Dunia(WB) , Bellla Bird alipongeza Mahakama ya Tanzania kwa juhudi zake za kujenga kituo hicho kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Mahakama na haki inapatikana kwa wakati.
Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama(IJA), Mhe. Jaji Paul Kihwelo alisema kituo hicho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa njia vedio kwa kushirikiano na IJA na Mbeya .
SOMA ZAIDI
Nice blog brother
ReplyDeletePost a Comment