Meneja Mkuu wa Shamba hilo Dk. Ahmed Eltigani Al Mansour alimueleza Rais Dk. Shein na ujumbe wake jinsi ya shamba hilo linavyofuga ngombe kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwemo kuwawekea viyoyozi na mafeni maalum kutokana na mazingira ya hali ya hewa ya ukanda huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Ahmed shamba hilo lina ng'ombe 12,500 ambapo kwa kila ngombe mmoja kwa siku hutoa lita 60 za maziwa na kutoa lita 250,000 kwa siku huku akitumia fursa hiyo kueleza siri ya mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na utafiti mkubwa walioufanya kabla ya kuazisha ufugaji huo.
Dk. Ahmeda alieleza kuwa ufugaji wanaoufanya ni ufugaji bora duniani na pia ni eneo lililopata mafanikio makubwa ikifananishwa na ufugaji unaofanyika katika maeneo mbali mbali zikiwemo nchi za Afrika na hata nchi zilizoendelea ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa wingi.
Akimaliza ziara yake katika eneo hilo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Al Rawabi kuwa Zanzibar itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo katika sekta hiyo ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kupanua wigo na kujifunza jinsi ya mafanikio hayo yalivyopatikana.
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment