Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kwa kushirikiana na team yake ya Mpoto Foundation alitembelea kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
Akizungumza akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.
“Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.” alisema Mpoto.
Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.
Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akigawa misaada kwa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akipata picha ya kumbukumbu katika kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akigawa misaada kwa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale jijini Dar es salaam leo.
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment