Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimkaribisha Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimuelezea jambo katika Ofisi ndogo zaWizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi na Programu za Ushirikiano wa Kikanda Kutoka Ofisi za Jumuiya ya Maziwa Makuu Burundi, Bw. Parek Madout kwa pamoja wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi na Programu za Ushirikiano wa Kikanda Kutoka Ofisi za Jumuiya ya Maziwa Makuu Burundi, Bw. Parek Madout
***************************
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika Bw. Aniefiok Johnson katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Johnson pia ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wadau wa uwekezaji nchini kushiriki Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji la Jumuiya linaloratibiwa na Jumuiya ya Maziwa Makuu. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 18-23 Machi mjini Kigali, Rwanda na kuhudhuriwa na washiriki takribani 1000Kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment