DC CHONJO AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI SHULE YA MSINGI MJI MKUU | Tarimo Blog


Na Farida Saidy, Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amekabidhi mifuko 50 ya Saruji (Cement)  kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mji Mkuu  kwa ajili ya ujenzi na ukarabati  wa madarasa  katika  shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Tukio hilo la kukabidhi  mifuko hiyo ya Saruji 50 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarsa,  limefanyika leo Februari 25,2020  katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mkuu.

Dc Chonjo, amekabidhi mifuko hiyo kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mji Mkuu na kupokelewa na Mwalimu  Mkuu wa Shule hiyo, Bi Grace Malya, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo, Afisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro,  Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Mhe. Maringo Madadi, Walimu wa Shule sambamba na Watendaji wa  Kata hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, DC Chonjo, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa kwa jitihada za kutafuta wadau na kufufua shule hiyo iliyokuwa ikielekea kufa lakini pamoja na shukrani kwa Mkuu wa Mkoa amewashukuru sana wadau Nashela Hoteli kwa kusaidia ukarabati wa madarasa mawili lakini pia amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood  kwa kuwa karibu na maendeleo ya Manispaa baada ya kukarabati madarasa mawili kupitia mfuko wa Jimbo na pesa zake binafsi zenye thamani ya shilingi Milioni 1 na laki 4.

Amesema maendeleo katika jamii yanaletwa kwa ushirikiano kati ya serikali  na wananchi kwa kusaidiwa na wadau mbalimbali  katika kufanikisha mahitaji muhimu.

Ameongeza kuwa,  Manispaa ya Morogoro  licha ya wanafunzi wote waliandikishwa darasa  la kwanza kuanza shule na wale waliofaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza kwenda Sekondari   lakini changamoto  iliyopo  ni  upungufu  wa vyumba vya madarasa katika upande wa Shule za Msingi pamoja na Sekondari.

"Tumeanza kuchukua hatua za kuboresha miundombinu yetu ya shule, Mhe. Diwani hii shule imebeba jina la Kata ni aibu kuwa katika hali hii , hivyo lazima muweke jicho la huruma katika shule hii, RC ameanza, Mhe. Mbunge ametusaidia , Wadau wakafuatia, na wewe ujitahidi katika vikao vyenu vya BMK (Baraza la Maendeleo ya Kata ) muwaambie wananchi kwamba tunahitaji michango wasio na watoto na wenye watoto wachange kwa kutofautiana viwango , na pia ikiwezekana mfuate Mstahiki Meya yule anawadau ukimlilia hawezi kuacha kukusaidia angalia mfano shule ya Msingi Mazimbu A na B wameshaa vikao wananchi wamechanga mimi nafika pale naenda kuoneshwa walichochanga ili kuoana wananchi wanapenda maendeleo na hata ukiwaona walimu wana haiba ya upendo wa kuwafundisha wananfunzi na hata na matokeo yake ni mazuri , usikake kimya sisi tunahangaika lakini nanyie muhangaike kama sisi " Amesema DC Chonjo.

Pia amemtaka Mhandishi wa Manispaa  pamoja na wahusika wanaopokea vifaa kutoka kwa Wadau kwamba wasivitumie mpaka pale nguvu ya wananchi wa Kata hiyo ya Mji Mkuu  itakapoonekana hayo ni maagizo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mhe. Loata Sanare ambaye yupo ziarani kikazi.

Amesema vifaa hivyo vinavyopokelewa vikitumika kimoja kimoja watashindwa kufikia lengo na kusudiao la ukarabati wa ujenzi  huo wa madarasa ,  hivyo vinatakiwa viwe vya kutosha ili ujenzi ukianza basi malengo yanakamilika na shule inaonekana  katika mazingira mazuri yenye miundombinu ya kuvutia kuanzia Jengo la Utawala la Ofisi ya Walimu ili kumfanya mwalimu kuwa na haiba ya kuwafundisha wanafunzi vizuri.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo, amepongeza mkuu  wa wilaya ya Morogoro  kwa kuunganisha  wadau  mbalimbali  katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuahidikutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa wa madarsa mengine yaliyobakia.

 Amesema kuwa kwa kutumia Saruji hiyo, itasaidia kuongeza nguvu  katika maeneo ambayo ujenzi wa madarasa unaendelea.

Naye Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Mhe. Maringo Hassan Madadi, amesema  mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule hiyo  inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi waliopo katika shule hiyo.


‘Tunaushukuru sana Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa pamoja na Wadau wa maendeleo  kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama mlivyokusudia katika ukarabati wa madarasa ya shule hii, lakini maagizo yaliyotolewa na Mkuu wetu wa Wilaya tutayafanyia kazi, tunaahidi tutakwenda kukaa na wananchi wetu na tutachangisha pesa ili tuendeleze maendeleo ya elimu katika kata yetu hususani shule hii ya Msingi ya Mji Mkuu ” amesema Mhe. Maringo

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mji Muu, Bi. Grace Malya, ameushukuru Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa , pamoja na Wadau wa Maendeleo huku akisema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyokusudiwa.

Amesema  shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa Ofisi ya Walimu  hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.


 Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo (kulia)akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mkuu, mifuko 50 ya Saruji.
 Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Mhe. Maringo Hassan Madadi akishikana Mkono na Mkuu wa Wilaya leo mara baada ya kumalizika zoezi la utoaji wa Saruji.
 Baadhi ya Wanafunzi wakishuhudia tukio la utoaji wa Saruji kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro leo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2