Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Usimamizi na Udhibiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Collins Nyakunga ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) kuwa na uelewa wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013, Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na.10 ya mwaka 2018, miongozo na Kanuni husika za Ushirika.
Mrajis ametoa wito huo akiongea na Viongozi pamoja na Watendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) wakati wa mafunzo ya Sheria Na.10 ya Huduma Ndogo za Fedha yam waka 2018 iliyofanyika Jijini Dar es salaam Hivi karibuni.
“Viongozi na Watendaji ni lazima kuzijua na kuzifuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Ushirika ili kuhakikisha kuwa mnatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na usahihi bila kukinzana na taratibu za Kisheria. Kwa kufanya hivyo, mtavisaidia vyama kuwa endelevu, kujenga na kuongeza imani kwa wanachama wenu,” alisema Nyakunga
Aidha, Mrajis amewataka viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kutoa taarifa rasmi pindi Ofisi za Vyama zinapohama au kubadili eneo la kazi. Akielekeza Viongozi wa Vyama kutoa taarifa kwa Mamlaka husika ikiwa ni pamoja na Afisa Ushirika, Mrajis Msaidizi wa Mkoa na nakala iwasilishwe Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kutunza kumbukumbu sahihi zitakazosaidia mambo mbalimbali ya Kiutendaji katika Ushirika. Hivyo, kuwataka Maafisa Ushirika na Warajis Wasaidizi kufuatilia taarifa kama hizo zinapotolewa.
Akizungumzia Uchaguzi katika Vyama vya Ushirika Mrajis amewakumbusha Viongozi na Watendaji kuzingatia suala la kufanya Chaguzi za Viongozi wa Vyama kwa mujibu wa Sheria, inayoelekeza Vyama kufanya Chaguzi kila baada ya miaka mitatu ya uongozi. Akisisitiza kufanya Chaguzi na kupata viongozi wapya ni njia bora ya kuwajengea uwezo wengine katika uongozi, kukuza vipaji na kuhakikisha uendelevu wa vyama. Hivyo, ameelekeza Vyama vyote vinavyopaswa kufanya chaguzi kutekeleza wajibu huo kwa mujibu wa taratibu ifikapo tarehe 30/06/2020.
Pamoja na mambo mengine Mrajis amewataka Viongozi, Watendaji wa Vyama kwa kushirikiana na Warajis Wasaidizi wa Mikoa pamoja na Maafisa Ushirika kufuatilia wanachama wenye madeni sugu ya Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo ili kuhakikisha kuwa mitaji ya Vyama inaendelea kuwa imara na kunufaisha wanachama wengi zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TRA SACCOS Bw. Joseph Wilbert amesema Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 inaenda kuleta tija zaidi kwa vyama vya Ushirika hususani Vyama vya Akiba na Mikopo kutokana na maelekezo ya usimamizi wa rasilimali za Vyama. Akiongeza kuwa Mafunzo hayo yaliyotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) yataongeza uwajibikaji kwa Vyama kwani yamewapa uelewa wa haki na Wajibu wao kama watendaji wa Vyama vya Ushirika.

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Kifedha Bw. Josephat Kisamalala akitoa mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wa SACCOS kuhusu Sheria Na.10 ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 yaliyoandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Jijini Dar es salaam
Mjumbe wa Mafunzo ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha akiuliza swali baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Usimamizi na Udhibiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw. Collins Nyakunga akiongea na Viongozi pamoja na Watendaji wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya Sheria Na.10 ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018. Mafunzo yaliyofanyika Jijini Dar es salaam Hivi karibuni
Afisa Ushirika Bw. Boniface Moshi akitoa mada kuhusu Sera na miongozo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha kwa Viongozi na Watendaji wa SACCOS, Jijini Dar es salaam
Wajumbe wa Mafunzo wakifuatilia mada na majadiliano mbalimbali wakati wa mafunzo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment