Na Amiri kilagalila,Njombe
WANANCHI wa kijiji cha Mikongo kilichopo kata ya Kifanya mkoani Njombe wamesema elimu zinazo tolewa na serikali kwa lengo la kuhamasisha vikundi imepelekea kuundwa kwa kikundi cha upandaji miti ambacho tayari kimeshapanda hekta 50 za miti ili kujikwamua kiuchumi pamoja na utunzaji wa mazingira.
Kikundi cha Kiwamiko chenye jumla ya wanakikundi 77 ambacho kilianza rasmi mwaka 2012 kimepata bahati ya kuwezeshwa miche ya miti na kila mwanakikundi anamiliki ekari tano za miti huku kikiwa na jumla ya hekta 50 licha changamoto wanazo kabiliwa katika uendeshaji wa zao hilo la misitu.
“Licha ya changamoto ya miti tunayokutana nayo lakini bado tunahamasika sana,mfano tukikutana na changamoto ya moto kwenye misitu yetu kijijini lazima Kijiji tuungane na utakuta wengine wanapika chakula wengine tukiendelea kuzima moto kwa kweli katika kilimo cha miti sisi wananchi tumehamasika sana”alisema Betrice Wogofya
Baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Mikongo Emmanuel Mgaya amesema kutokana na changomoto ya uchomaji moto zimewekwa sheria za kukabiliana na janga hilo huku mwenyekiti wa kikundi cha Kiwamiko Kastori Mkalawa akisema zao la miti limekuwa chachu ya maendeleo kwa baadhi ya wananchi kijijini hapo.
“Mpaka sasa tumefanikiwa kupanda hekta 50 ambazo zinauwiano wa kila mtu kuwa na hekta kama tano,lakini bado huwa kuna changamoto hata kama sisi wananchi tumehamasika kwenye kilimo cha miti”
Kutokana na mwamko huo mkuu wa wilaya ya Njombe ameungana na wanakikundi cha Kiwamiko kupanda miti katika shamba darasa ili wanachi wengine wajifunze kupitia shamba hili huku akihamasisha uanzishawaji wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa zitokanazo na miti.
“Mimi naona imefika mahala tutafakari tunaweza kutengeneza hata kiwanda kidogo, kwa mfano cha kupaki njiti za viberiti na baadaye mnaweza kupeleka kwenye viwanda vya viberiti ili kuweka risasi lakini pia kutengeneza vijiti vya meno na vitu vingine vidogo vidogo vinavyoweza kutumika ndani au nje ya maeneo yetu”Alisema Msafiri
Zaidi ya miti 1000 imepandwa na wanakikundi katika shamba hilo ili kuendelea kuhamasisha kilimo cha miti kwa wananchi.
Baadhi ya wanakikundi cha Kiwamiko wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri kabla ya zoezi la upandaji wa miti kwenye shamba darasa.
Wa pili kutoka kushoto ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akitoa mche wa mti kwenye kiriba kama zoezi la uzinduzi wa upandaji miti kwenye shamba darasa.
Mche wa mti ukiwa tayari umepandwa kwenye ardhi katika shamba darasa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment