KANISA KUGAWA BARAKOA KWA WAUMINI WAKE | Tarimo Blog

Na Editha Karlo,Kigoma.

Katika kupambana na maambukizi ya virusi vya  ugonjwa wa Corona (Covid 19), Paroko wa parokia ya Mt. Vicent wa Paulo Katubuka jimbi la Kigoma Padre  Stephene Shaiju amesema kanisa limeandaa mkakati wa kuhakikisa kila muumuni anapata barakoa 2 bure kutokana na barakoa kuuzwa bei ambayo siyo kila mtu anaweza kuimudu.

Ameyasema hayo wakati wa misa takatifu iliyoazimishwa parokiani hapo baada ya Daktari kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

Padre Shaiju alisema Kwa hali halisi ya kipato vyetu siyo kila mmoja ataweza kumudu ghalama ya kununua barakoa hivyo kuwaomba waamini waunge Mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia kila mmoja anachojaaliwa ikiwa mahitaji ni ujuzi, vifaa ambavyo ni vyerehani na vitambaa.

"Tunajua hali zetu, niwaombe ndugu waamini tuungane katika hili, mwenye cherehani alete, mwenye uwezo wa kununua vitambaa alete na masisita wetu watatuelekeza namna ya kushona barakoa, lakini pia daktari atatuelekeza kitambaa sahihi" alisema Padre Shaiju.

Awali akitoa Elimu kwa waamini hao Mkurugenzi wa Hospitali ya Kabanga iliyopo wilayani Kasuku Dkt. Peter Mayengo alisema tukizingatia Maelezo yanayotolewa na serikali kupitia wataalamu wa afya tutaweza kuepuka janga hili.

Ambapo alikumbushia taratibu hizo kuwa ni kuacha mikusanyiko isiyo ya lazima,  kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji turirika kwa sekunde zisizopingua 20, kutumia barakoa kwa sahihi, kutojigusa sehemu za tunazoelezwa na wataalamu kwa kuwa ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya hewa.

Naye askofu wa jimbo katoriki Kigoma Askofu Joseph Mlola ametoa wito kwa wazazi kuwalinda watoto wao kwa  kipindi hiki kwa kuwa hawatambui madhara ya ugonjwa huu na kuwazuia wabaki majumbani.

Baada ya shule kufungwa baadhi ya wazazi wameaacha watoto wanarandaranda mtaani hali ambayo ni hatari na kuwataka watambue kuwa aliyefunga shule alikuwa na maana ya kuwalinda watoto.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2