MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE TATU ZA KUSAFISHA DAMU HOSPITALI YA AMANA ILI KUHUDUMIA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO WALIOAMBUKIZWA UGONJWA WA CORONA | Tarimo Blog


Mojawapo ya mashine ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo iliyofungwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ambayo thamani yake ni TZS. 70 Mil.


Mashine ya kusaidia mgonjwa kupumua ambayo itafungwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ambayo thamani yake ni TZS. 56 Mil.

Mtambo wa kuchuja maji (Portable RO System) kwenda kwenye mashine ya kusafisha damu wenye thamani ya TZS. 28 Mil uliofungwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefunga mashine tatu za kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo zenye thamani ya TZS. 210 Mil. na inatarajia kufunga mashine moja ya kusaidia mgonjwa kupumua (ventilator) yenye thamani ya TZS. 56 Mil. katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ili kuhudumia wagonjwa waliopata maambukizi ya virusi vya CORONA.

Tayari wagonjwa wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa na wafanyakazi wa MNH waliopo Hospitali ya Amana tangu Ijumaa ya tarehe 24 Aprili, 2020 saa 12 asubuhi ambapo dawa na vitendanishi vya kutoa huduma ya kusafisha figo kwa sasa vinagharimiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Sambamba na hilo, Hospitali imefunga mtambo wa kuchuja maji (Portable RO) wenye thamani ya TZS. 28 Mil. na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi ya kusafisha damu uliogharimu TZS. 12 Mil. Kutokanana hilo, MNH itapokea madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana kuanzia tarehe 28 Aprili, 2020 ili kujengewa uwezo kwenye Kitengo cha Kusafisha Damu pamoja na vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICUs) aina tano tofauti.

Aidha, MNH kupitia Hospitali ya Upanga na Mloganzila, ilipokea wagonjwa 93 kutoka Amana wakiwemo watoto wachanga 30 chini ya mwezi mmoja wakiwa na mama zao, watoto wanne chini ya miaka mitano, kina mama wajawazito 36, wagonjwa wa upasuaji 10 na wagonjwa 13 wenye magonjwa ya ndani (internal medicine).

MNH imekua bega kwa bega na Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye maandalizi ya kupokea wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona katika Hospitali Rufaa ya Amana ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wagonjwa waliolazwa wanapata huduma. MNH inatoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kujinga na kuwakinga wengine kulingana na maelekezo yanayotolewa na Serikali.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2