KATAVI YAPOKEA VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA | Tarimo Blog


* RC KATAVI  ATOA SAA 48 KWA MCHINA ALIYEKATAA KUNAWA AFIKISHWE MAHAKAMANI.


Serikali Mkoani Katavi imepokea Vifaa tiba kwa ajili ya kuendelea na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona ikiwemo vifaa vinavyotumika kupima joto la mwili ambapo ni miongoni mwa changamoto iliyokuwa ikiukabiri Mkoa huo huku Mkuu wa Mkoa wa Katavi akitoa masaa 48 kwa Jeshi la Polisi kumfikisha Mahakamani Raia wa Kichina aliyekataa kunawa mikono yake maji tiririka.

Akipokea Vifaa hivyo kutoka Water Reed Program wanaojihusisha na masuala ya Ukimwi,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Juma Homera ameshukuru kwa masaada huo na kuomba wadau kuendelea kusaidia pamoja na kulitaka Jeshi la Polisi kumfikisha Mahakani Lin Guosong Raia wa Kichina ambae ni Mfanyabiashara aliyekataa kunawa Mikono yake kwa maji tiririka.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Omari Sukari anabainisha kuwa kupatikana kwa vifaa hivyo kutasaidia kupubguza changamoto iliyokuwa ikiwakabiri ya vifaa dhidi ya mapambano ya Ugonjwa wa Corona.

Awali akikabidhi vifaa hivyo Mratibu wa Mkoa Katavi kutoka  Taasisi ya Water Reed Program Shaban Ndama ameeleza adhima yao ya kuendelea kusaidia Mkoa huo katiuka Mapambano dhidi ya Mlipuko wa Ugonjwa wa homa ya Mapafu COVID 19.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2