HAZINA: MKURUGENZI Mtendaji Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Nyamajeje Caleb Weggoro, akipokea Kitabu cha MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY kutoka kwa mwandishi wake, Derek Murusuri, jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii.
Dkt. Nyamajeje alikuwa anawakilisha mataifa nane (8) ya Afrika katika Bodi ya Wakurugenzi ya AfDB.
Nchi hizo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Seychelles na Sudan ya Kusini.
Dkt. Nyamajeje ambaye amefurahishwa na ujio wa kitabu cha MAKING AFRICA WORLD'S LARGEST ECONOMY, amesema kwamba ili kuhamasisha maendeleo ya Afrika, ni muhimu kwa waafrika kuandika habari zetu wenyewe (telling our own stories) na kuona fahari kutengeneza mashujaa wetu ili kuimarisha ujenzi wa jamii imara barani zitakazojiletea maendeleo zenyewe badala ya kuendelea kuyategemea mataifa wahisani.
Dkt Nyamajeje ambaye pia aliwahi kuwa Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala ya Uchumi na Utangamano wa Mataifa ya Afrika, vilevile alikuwa miongoni mwa viongozi walioisuka upya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amewashauri watanzania kujenga utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu ili kutunza na kuijua historia yao, ambayo ni muhimu katika kuhifadhi urithi wetu.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment