LHRC KUZINDUA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA 2019 KWA NJIA YA MTANDAO | Tarimo Blog

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wametangaza kupitia tovuti yao na mitandao ya kijamii kuzindua Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019. 

RIPOTI imepangwa kuzinduliwa Jumatano, Aprili 29, 2020 kupitia mtandao wa YouTube (Haki TV), mtandao wa Zoom na mitandao ya Twitter, Facebook na Instagram.

 Kwa mujibu wa LHRC, hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la utetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuzindua ripoti kwa njia ya kidigitali tangu walipoanza kuchapisha ripoti hiyo mwaka 2002.

LHRC imetaja sababu kubwa ya kulazimika kufanya hivyo ni kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao umewalazimisha kufanya kazi kutoka nyumbani na kuepuka mikusanyiko ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo ripoti hiyo itaangazia hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2019 sambamba na kufanya ulinganisho wa hali ilivyokuwa mwaka 2018. Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania inayoandaliwa na LHRC huangazia haki zote za binadamu ikiwemo haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi, haki za maendeleo na haki za makundi maalumu.

Ripoti hiyo pia huchambua ufanisi wa mamlaka za usimamizi wa haki na kutoa mapendekezo kwa lengo la maboresho.

Tumia link hizi Haki TV kufuatilia moja kwa moja uzinduzi huo kuanzia saa 4:00 asubuhi kupitia mtandao wa You Tube   na mtandao wa Zoom

 (Bofya <<Hapa>> Kuingia Zoom
  au Bofya <<Hapa>> kuingia You Tube) ↡↡


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2