WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA KUTOKA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) | Tarimo Blog



Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 28/04/2020.
WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mbali mbali vya kuthibiti maambukizi ya Corona kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110.

Akipokea msaada huo, huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Jamala Adam Taib amelishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada ambao utawasaidia wafanyakazi kutekeleza kazi zao kwa ufanisi pamoja na kujikinga na maambukizi ya Corona

Alifahamisha kuwa Shirika la Afya Duniani linaendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuonyesha mashirikiano ya pamoja katika udhibiti na ufuatiliaji wa mwenendo mzima tokea mwanzoni mwa Mripuko wa maradhi hayo kuanza .

Nae Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Ghirmay Ande Michel wakati akikabidhi vifaa hivyo amesema vifaa hivyo vimekusudiwa kutumika katika kitengo cha mwenendo wa Kuratibu Maradhi ya Mripuko yakiwemo (COVID -19).

Amesema vifaa hivyo ni vitendea kazi ikiwemo komputa za kisasa vifaa vya thamani,Barakoa,vipima joto ,cloves,nguo maalumu za kujikinga na maambukizi ya maradhi ya Corona na vyenginevyo .

Alifahamisha kuwa Shirika la Afya Duniani litaendelea kutoa misaada mbali mbali ya kujikinga na maambukizi ya Corona na (COVID-19) Kwa lengo la kupambana na mripuko huo ambao umeikumba Dunia.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2